China yaziongoza nchi kubwa duniani kuratibu uhusiano na nchi za Afrika

China yaziongoza nchi kubwa duniani kuratibu uhusiano na nchi za Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
d439b6003af33a870885278ab7a8e9325143b5b1.jpeg


Katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya China na nchi za Afrika umekuwa ukifuatiliwa na nchi nyingi duniani. Ufuatiliaji huo umekuwa na malengo tofauti, kuna ule unaotokana na kuiga mtindo wa China wenye uratibu mzuri na maendeleo ya kunufaisha kati ya China na Afrika, na mwingine una malengo ya kukwamisha hata kuupaka matope uhusiano kati ya China na nchi za Afrika. Lakini kwa mtazamo wa jumla, kinachoweza kuonekana ni kuwa uhusiano kati ya China na Afrika umefanya ufuatiliaji wa nchi kubwa kwa bara la Afrika uongezeke.



Kwa muda wa miaka 22 tangu Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) lianzishwe, kumekuwa na mafanikio mengi kwenye sekta za uchumi na diplomasia kati ya China na nchi za Afrika. Kumekuwa na ongezeko kubwa la thamani ya biashara kati ya pande mbili, ambalo limechochea ongezeko la uchumi katika nchi za Afrika, na pia kumekuwa na ukaribu zaidi kidiplomasia kati ya China na nchi za Afrika kwenye siasa za kikanda na hata kimataifa. Msingi wa ushirikiano na matokeo yake kwa pande hizo mbili umeonesha kivitendo dhana ya ushirikiano wa kunufaisha.



Hali hii imevutia ufuatiliaji wa baadhi ya nchi kubwa duniani, kila moja ikiwa na malengo yake. Baadhi ni zile ambazo hazifurahishwi kuona nguvu yao ya ushawishi ya muda mrefu na mirija yao ya kiuchumi, inaanza kupotea baada ya nchi za Afrika kuwa na mbadala wa uungaji wenye uhakika. Na nyingine ni zile zinazotaka kunufaika na fursa za kiuchumi zinazoonekana sasa kutokana na maendeleo yanayopatikana barani Afrika.



Umoja wa Ulaya kwa mfano umeweka utaratibu wa mkutano wa kilele na Umoja wa Afrika (EU-AU Summit) tangu mwaka 2000, ambao licha ya kutaja kuwa lengo lake ni kuendeleza uhusiano wa kihistoria kati ya pande mbili, sehemu nyingine kuhimiza maendeleo ya kiuchumi. Lakini ukiangalia undani ya uhusiano huo, ni kulinda maslahi zaidi ya Umoja wa Ulaya, na ukilinganishwa na FOCAC bado haujaweza kuonesha maendeleo kama yanayoonekana kwenye uhusiano na China kwenye biashara, ujenzi wa miundombinu na hata uwekezaji. Hata hivyo ili kutoachwa nyuma na China Umoja huo umeonekana kujitahidi kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika.



Nchi nyingine pia zimeanzisha utaratibu kama wa FOCAC. Mwaka 2008 India ilianzisha utaratibu wa kuwa na mkutano wa kilele na viongozi wa nchi za Afrika (India-Africa Summit), mwaka 2014 Marekani ilianzisha utaratibu wa mkutano wa kilele na nchi za Afrika, Japan pia imekuwa ikiimarisha ushirikiano kati yake na nchi za Afrika kupitia utaratibu wake wa TICAD.



Nchi za Afrika zikiwa ni wanachama wa harakati ya kutofungamana na upande wowote, zimekuwa zikikaribisha ushirikiano na nchi mbalimbali duniani, iwe ni kwa utaratibu kama huo wa mikutano ya kilele ya viongozi wakuu, au uhusiano kati ya nchi na nchi. Ni jambo zuri kwa utaratibu wa FOCAC kuleta msukumo wa ushirikiano kati ya Afrika na sehemu nyingine duniani. Hasa kuipa maana kauli ya “ushirikiano wa kunufuaishana”, ambayo China imekuwa ikitekeleza kivitendo.



Lakini bahati mbaya ni kuwa baadhi ya nchi ni kama zinaanza kuchukulia ushirikiano na nchi za Afrika, kuwa ni jukwaa la kushambulia ushirikiano kati ya China na Afrika kwamba wao wanaleta ushirikiano ulio bora. Maana halisi ya ushirikiano bora kati ya bara la Afrika au nchi yoyote ya Afrika na nchi nyingine, itaonekana kama kweli ushirikiano utakuwa ni wa kunufaishana au ni wa kunufaisha upande mmoja. Kwa sasa sio vigumu kwa nchi za Afrika kutambua uhusiano upi una manufaa kwa nchi hizo na upi hauna manufaa.
 
Back
Top Bottom