ChinaTech: Italy walijitoa katika BRI ya China, hatimaye Waziri Mkuu wa Italy atembelea China kuomba kurudisha tena ushirikiano kati ya mataifa hayo

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Mwanamama Giorgia Meloni alishinda uchaguzi mkuu wa Italy mwaka 2023 na kuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo ambalo pia ni member wa G7 na NATO.

Alipoingia tu madarakani, kwa shinikizo la Marekani na mataifa mengine ya Ulaya akaiondoa Italy kutoka kwenye mpango wa China unaoitwa BRI na kumkosoa mtangulizi wake, waziri mkuu mstaafu Giussepe Conte aliyesaini mkataba huo na China mwaka 2019.

Lakini sasa Waziri Mkuu huyo Giorgia Meloni ameanza kuona umuhimu wa China na anataka "kuanza awamu mpya" ya ushirikiano kati ya Rome na Beijing.

Jumamosi 27 July 2024 aliwasili China na atakuwa na ziara ya siku tano. Jumapili 28 July alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Li Qiang.

"Italy ina nia ya kuanza awamu mpya, kuzindua upya ushirikiano wetu baina ya nchi hizi mbili.”
Giorgia Meloni (PM Italy)​


Pia ameshiriki kongamano la kibiashara na kutia saini ushirikiano wa miaka 3 katika sekta mbalimbali za kiteknolojia na kibiashara ambazo China imekuwa ikifanya vizuri:
  • Ship building​
  • Aerospace​
  • Electric Vehicles (EVs)​
  • AI technology​

Meloni alisema wanatambua kuwa Italy haina uwiano sawa wa kibiashara na China (trade deficit) hivyo akaomba Italy ipate nafasi zaidi katika soko la China.



Italy inakabili trade deficit katika biashara na China, inanunua bidhaa nyingi za China kuliko inavyouza bidhaa zake China.


Katika kongamano la biashara kati ya China na Italy, Meloni aliongozana na wawakilishi wa makampuni ya Italy kama vile kampuni kubwa ya kutengeneza matairi ya Pirelli, energy group ENI (zamani iliitwa Agip), defence group Leonardo, makampuni ya luxury fashion kama Dolce & Gabana, watengenezaji wa wine n.k.

Jumatatu anatarajia kufanya mazungumzo na raisi wa China, Xi Jinping.


Miaka hii ni ngumu sana kuikimbia China katika biashara, teknolojia na infrastructure.
Who's next European leader will visit China? Lets wait and see!
 
Ngoja waje wamerekan wa maji matitu
 
Ngoja waje wamerekan wa maji matitu
Ni hadimu sana kiongozi mkubwa kuwa na ziara ya siku 5 kwenye taifa lingine

Ni ziara ndefu sana amelazimika iwe hivi ili kuwaplease Wachina

Mara zote Xi Jinping anayaambia mataifa ya Ulaya wawe na win-win cooperation na China wao wanamsikiliza Marekani ndio haya ya Italy yanawakuta
 
Du aisee ,Dunia inaenda Kasi sana
Dunia inaenda kwa kasi sana, chukulia mfano tu kwenye EV

●Siku za karibuni Trump kwenye kampeni zake alisema milango iko wazi kwa Wachina kuwekeza Marekani kwenye EV akichaguliwa raisi wa Marekani.





●Xi Jinping alipotembelea Ufaransa, waziri wa uchumi wa Ufaransa naye alisema kama Trump




●Juzi kati BYD wameingia mkataba na Uturuki kuanzisha kiwanda cha EV


Ni Wamarekani wa Buza tu ndio ambao wanaichukulia poa China.
 
Una muamini Trump ?
Trump alichoongea alimaanisha.

China imewekeza sana Mexico, siku hizi bidhaa nyingi za China zinaingia Marekani kupitia Mexico ikiwa kama third party.

Na kuna kampuni ya China ya kutengeneza EVs ina mpango wa kufungua kiwanda Mexico, Trump akasema hayo magari ikiwa yataingia Marekani kutoka Mexico atayawekea tariffs kubwa

La sivyo hizo kampuni za Kichina zikafungue factories Marekani ili zisikumbane na hilo rungu la tariffs atakapokuwa raisi

Technical know-how aliyo nayo Mchina kwenye EV ni kubwa zaidi ya Marekani

U.S wanahitaji EV tech transfer kutoka China.
 
Kuna mbuzi watakwambia China kuwa hivyo kataka Marekani,na Marekani akiamua anaweza kuishusha ChinaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
 
Ndio maana mwenyekiti wa EU Bi.Ursula alisema kweli kuwa China sio taifa la kukinzana nalo bali la kukubaliana nalo.Hii kauli aliongea kipindi China na US wana mvutano juu ya Taiwan.
Kuna huyu Bi. Ursula na U.S Treasury Secretary Bi. Janet Yallen kuna wakati ushabiki wanaweka pembeni wanaongea ukweli kuhusu China

Inaonekana wamama ni ngumu sana kukaza kwa China hilo limeonekana kwa Ursula, Janet, Meloni

Sasa Marekani wajichanganye wamchague Kamala Harris awe raisi
 
Ngoja tuone itavyokua.
 
China kama mma ila kuna wamarekani wa jf ngojea watakuja hapa hapa
Shida wanasiasa kuna mambo hua wanayaamua kisiasa badala ya kitaalamu matokeo yake ndio kama haya sasa
Ila yote kwa yote Belt and road initiative alobuni hii projects hapo china dunia na wachina wenyewe watamkumbuka vizazi na vizazi kwakweli
 
Mataifa ya Eastern Europe na Middle East pamoja na Asia Pacific kwa wingi sana wamejiunga na BRI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…