Uchaguzi 2020 Chini ya CHADEMA, elimu ya msingi itakuwa miaka tisa

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
16,054
Reaction score
11,568
Nimeisoma ilani ya CHADEMA sura ya tano ibara ya saba kifungu "e" nimekiambatanisha hapa chini, kinasema ili kuboresha elimu shule ya msingi itakuwa miaka tisa, binafsi ningependa shule ya msingi iwe miaka mitano, lengo la shule ya msingi kama lilivyo ainishwa na Friedrich Froebel ni kumuandaa mtoto kuanza maisha ya elimu na sio kumpa stadi za maisha.

Halafu kifungu "f" wanasema wata integrate na elimu ya ufundi yaani mwanangu anapenda kuwa daktari unaanza na kumfundisha uchomeleaji vyuma, naona sio sawa. Hebu tuiache elimu kama ilivyoasisiwa na akina Friedrich Froebel na Johann Friedrich Oberlin. Pamoja na kasoro ndogondogo ilani ina mambo mazuri pia ni bora wakatumia muda wao kuyaelezea.
1599043582741.png
 
Chadema ni wababaishaji tu, kila mtu akisimama jukwaani utasikia, "Risasi 16" mara risasi 64 bado zingine zimo kiunoni, yaani maajabu tu. Jana mke wa mgombea wao kasema tena huku anatoatoa vimachozi mambo hayo hayo ili wananchi wamuhurumie!! hakuna kura za huruma hapa, mtu ukae ulaya upangwe na mabeberu kuja nchini kutaka kubaka kura kwa kigezo cha huruma
 
..nadhani jambo la msingi ni kuangalia toka darasa la kwanza mpaka kujiunga chuo kikuu ni muda gani.

..mifumo ya elimu iko ya aina mbalimbali lakini kikubwa ni kuangalia kipengele nilichokitaja hapo juu.

..ila ELIMU ni suala nyeti sana na ni muhimu kuwa makini nalo, na kuwaachia WATAALAMU watuongoze.

..ningependa CDM waeleze wanataka elimu ya Mtanzania iwe vipi, halafu wataalamu waje na mpango wa utekelezaji.
 
Huyu jamaa yenu, inje ya kushuhudia kiki za miujiza kwa upande wa kiutawala ni mweupe kichwani. Yeye angeambiwa asome hiyo miaka Tisa angefika hapo alipo mapema??
 
Kwa hiyo hakupigwa risasi? Au unataka kusema nini? Subiri na wewe waje wakugonge moja tu ya kiuno tuone kama utaendelea kuropoka.
 
Huyu jamaa yenu, inje ya kushuhudia kiki za miujiza kwa upande wa kiutawala ni mweupe kichwani. Yeye angeambiwa asome hiyo miaka Tisa angefika hapo alipo mapema??

..toka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu ni miaka mingapi?

..hilo ndilo suala la msingi na kuuliza hapa.

NB:

..kuna nchi shahada ya kwanza ni miaka 3.

..kwingine shahada ya kwanza ni miaka 4.
 
..nadhani jambo la msingi ni kuangalia toka darasa la kwanza mpaka kujiunga chuo kikuu ni muda gani.

..mifumo ya elimu iko ya aina mbalimbali lakini kikubwa ni kuangalia kipengele nilichokitaja hapo juu.

..ila ELIMU ni suala nyeti sana na ni muhimu kuwa makini nalo, na kuwaachia WATAALAMU watuongoze.

..ningependa CDM waeleze wanataka elimu ya Mtanzania iwe vipi, halafu wataalamu waje na mpango wa utekelezaji.
Hawajasema kwahiyo itabaki hivyohivyo 4-2-4
 
..miaka 4 chekechea.

..miaka 5 darasa la kwanza.

..na hii itaokoa watoto wengi wa kike.

una miaka 4 uko chekechea???? mtu ana miaka 16 ashaanza kupokea mshahara mbele, wengine washasajiliwa mpaka club kubwa! kwan mna kwama wap cdm
 
..toka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu ni miaka mingapi?

..hilo ndilo suala la msingi na kuuliza hapa.

NB:

..kuna nchi shahada ya kwanza ni miaka 3.

..kwingine shahada ya kwanza ni miaka 4.
Hiyo miaka Tisa watasomesha watoto wao. We we unazungumzia chuo kikuu au primary,
Hizo inchi wenzio wako chuokikuuu, usikute huo umri wa miaka Tisa ndo wenzio wako chuo Kikuuu, halafu unataka watoto wauswahilini wazeekee primary?
 
..Nimeuliza toka shule ya msingi mpaka chuo kikuu ni miaka mingapi?

..ukiweza kutupatia majibu ndiyo sasa tutaweza kusema vijana wetu watazeekea mashule au la.
 
una miaka 4 uko chekechea???? mtu ana miaka 16 ashaanza kupokea mshahara mbele, wengine washasajiliwa mpaka club kubwa! kwan mna kwama wap cdm

..hao ni wale ma-GENIOUS.

..mtoto wa kawaida anakwenda hivyo nilivyokueleza.

..sisi miaka yetu watoto walikuwa wanaanza darasa la kwanza wakiwa na miaka 9.

..tulikuwa tunapimwa kwa kushika sikio; mkono wa kulia uguse sikio la kushoto ndipo uandikishwe shule.
 
Back
Top Bottom