Uchaguzi 2020 Chini ya CHADEMA, elimu ya msingi itakuwa miaka tisa

sera ya elimu ya taifa ya mwaka 2014 inataka primary education watoto wasome kwa miaka 9 mpaka 10 sasa wewe unapinga pinga tu bila kujua sera ya elimu ya taifa?
 
mkuu, wakati wa nyerere tulikuwa na shule kama Dar Tech, Arusha tech, Mbeya tech, Ifunda tech, Shy com, hizi ulikuwa unaishia form four unaenda hizo shule, akaja jamaa mmoja anaitwa Mungai akabadilisha vyote vikawa Universities,
 
..halafu ccm inataka kurudisha JKT.

..Ni afadhali vijana wafundishwe ufundi na stadi nyingine mashuleni ili kusiwe na ulazima wa kwenda JKT.
Kuna mtu nimemuuliza,anaelewa nini maama ya "elimu ya msingi". Ukielewa dhana ya kuwa na miaka 9 ya elimu ya "msingi",utaelewa kuwa yale ambayo ungetakiwa kwenda kuyapata kwingineko kama JKT,utayapata kwenye elimu ya "msingi".
 
sera ya elimu ya taifa ya mwaka 2014 inataka primary education watoto wasome kwa miaka 9 mpaka 10 sasa wewe unapinga pinga tu bila kujua sera ya elimu ya taifa?
hapo anaanza shule akiwa na miaka mingapi? hii hii saba?
 
kama wanatuletea sera zilezile za ccm si bora tuendelee na ndalichako tu, kuliko hizi ilani za kupiga chabo
 
hapo anaanza shule akiwa na miaka mingapi? hii hii saba?
Kumbe unaropoka tu hata sera ya elimu ya nchi huijui ?

Mtoto anaanza elimu ya msingi shule ya awali ambayo 2 years hivyo anaanza akiwa na miaka mitano.

Lakini sera ya sasa imeunganisha primary school na secondary education kwa mfumo wa
1+6+4+2+3/4/5.

Hivyo suala la ilani ya CHADEMA limezingatia sera ya elimu ya taifa na mikataba ya kimataifa hasa UNESCO na ILO.

kama hujui kasome upya sera ya elimu
 
nivizuri elimu ya msingi iwe nimiaka 9 wafute form 5 na 6
 
....lastad na elim liko poa sana
 
mkuu, wakati wa nyerere tulikuwa na shule kama Dar Tech, Arusha tech, Mbeya tech, Ifunda tech, Shy com, hizi ulikuwa unaishia form four unaenda hizo shule, akaja jamaa mmoja anaitwa Mungai akabadilisha vyote vikawa Universities,
Kuna rafiki yangu mmoja(nikama mzee wangu) anawadhifa jeshini nilikua naongea juzi,akawa ananiambia kuwa Mungai alikua anatumiwa nawakenye kuharibu mfumo wetu wa elimu. Sijui kuna ukweli ndani yake.
 
sera ya elimu ya taifa ya mwaka 2014 inataka primary education watoto wasome kwa miaka 9 mpaka 10 sasa wewe unapinga pinga tu bila kujua sera ya elimu ya taifa?
Mtu mpaka anahitimu chuo kikuu itamchukua miaka mingapi?.

Kwa nini kama nchi tusifaate mfumo waelimu wa India?. Maana naona umekaa vizuri.
 
Hii sera bado iko kwenye mapitio, alternatively ulikuwepo mpango wakufanya elimu ya secondary kuwa universal yaani mtihani wa darasa la saba usiwe wa kuchuja uwe ni kipimo tu chauelewa kama ilivyo mtihani wa darasa la nne au form two. kusema mtoto aanze darasa la kwanza na miaka minne kimsingi huyu mtoto hajakomaa kuchanganyana na watoto wakubwa, hata kwenye school bus watoto wa kindergarten hawachanganywi na wa primary.
 
kama wanatuletea sera zilezile za ccm si bora tuendelee na ndalichako tu, kuliko hizi ilani za kupiga chabo
CCM wameshindwa kuitekeleza sera mpya badala yake wameiweka kwenye shelve.

Lakini chamsingi sana ni kuangalia namna gani wamelenga kuweka mambo muhimu at each stage ya mtoto kupata maarifa sahihi.

CCM imewashinda kuboresha elimu kuhakikisha inazalisha watoto wenye maarifa kutokana na kukosa miundo mbinu sahihi na utekelezaji wa sera umekuwa tia maji tia maji.

Mpango wa MMEM ulikuwa na lengo la kuongeza access to education limefanikiwa kwa asilimia Mia moja hongera kwa serikali lakini wamecompromise quality.

Sera ya elimu ya 1996 na 2007 ziliathiri kwa kiwango kikubwa sana quality na CHADEMA sambamba na kubadili mfumo na kuendana mfumo wa sera mpya wamelenga kuboresha kwenye maeneo ambayo ccm walifeli.

Unakumbuka mpango wa TBT chini ya professor Maghembe ulivyohujumiwa na wapinzani wake ?

Utekelezaji wa sera wa elimu wa ccm umefeli imagine watoto wanafundishwa TEHAMA kwa picha ya TV za chogo ambazo technology imeshazitupa tayari ???!!
 
Pilot phase iliyowekwa na sera imeshapita alipoingia ndalichako akaitupa ile sera kwa tamko binafsi tu.

Hivyo usiwanange chadema hatujaandaa ilani kwajili ya kuwageuza watanzania punching bags kama anavyofanya ccm.
 
Acha chuki maadili mada please hapa tunajadili issue ya kitaifa huwezi kaa kimya acha lipite
 
Mtu mpaka anahitimu chuo kikuu itamchukua miaka mingapi?.

Kwa nini kama nchi tusifaate mfumo waelimu wa India?. Maana naona umekaa vizuri.
Mkuu sera ya elimu is not a copy paste affair lazima ufanye utafiti ujiridhishe kwa kufuata falsafa na sera za nchi.

Elimu inapaswa kuwa zao la jamii na sera lazima zilireflect jamii husika.
 
Huyu jamaa yenu, inje ya kushuhudia kiki za miujiza kwa upande wa kiutawala ni mweupe kichwani. Yeye angeambiwa asome hiyo miaka Tisa angefika hapo alipo mapema??
Kiuhalisia elimu ya msingi kwa sasa ni miaka tisa. Shule zote za msingi zilipewa mwongozo wa kuwa na madarasa ya awali ambamo mtoto husoma mwaka 1 au 2 kulingana na umri na uelewa kabla ya kuifikisha miaka 7 kuanza darasa la kwanza.
 
Mtu mpaka anahitimu chuo kikuu itamchukua miaka mingapi?.

Kwa nini kama nchi tusifaate mfumo waelimu wa India?. Maana naona umekaa vizuri.
Sisi kama nchi huru kuna mambo tunapaswa kujisimamia kama nchi kama tulivyojisimamia kwenye corona, sio research zifanyike Bangladesh na Nepal sisi tumeze tu kama dodoki.

Kafilipino kenye miaka 15 utafikiri kana miaka minne, sisi mtoto wa mika tisa keshaanza kuota chuchu, sio mtu aende kwenye kongamano unesco kwa wazungu atuletee kabrash tumeze, hapana.

Hawa chadema wasitake kujipendekeza kwa wazungu kuonyesha wana comply, hapana, lazima tutathimini mazingira tuliyo nayo, mtoto unakomaa nae Feza boys au Marian unatamani asome miaka minne amalize shule namna ada inavyokupeleka mchakamchaka.
 
..toka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu ni miaka mingapi?

..hilo ndilo suala la msingi na kuuliza hapa.

NB:

..kuna nchi shahada ya kwanza ni miaka 3.

..kwingine shahada ya kwanza ni miaka 4.
Inategemea shahada ya fani gani, na anaechukua katoka level gani. Kuna nchi hawana A- level. Pengi, shahada ya kwanza ni kati ya miaka 3-5.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…