Chini ya utawala wa Magufuli, Taifa limepata hasara ya mabilioni na pia upotevu mkubwa wa fedha uliozua utata

Stupid! Cooked stories from same people. Tunajua Chadema mliumia na mengi ila hapa hatutoangalia sura bali nani anasimama na ukweli bila hila. Mtaelewa baadae ...

Nilijua na wewe ni CHADEMA. Sio?
 

Bila shaka ukinikabidhi shillingi milioni 100 nikujengee nyumba, nikajenga ya milioni 50 na kukukabidhi, utaipokea na kunisifu sana kwa vile nyumba “unaiona”, sio?
 
Uwazi na uhuru wa vyombo vya habari pamoja na bunge imara lisiloingiliwa na serikali vilifanya ujue haya yote chini ya jakaya. Ila awamu ya tano tumeona vyombo vya habari na upinzani ukiminywa pia uwazi ulikosekanika kabisa. Tungeyajulia wapi hayo hakuna ruhusa hata ya kufanya takwimu wala mikutano ya kisiasa.
 

Aisee. Nimeona hoja yako kwamba JPM alituibia naye lakini alituletea maendeleo. Sawa.

Tatizo linalojitokeza sasa ni kuwa aliingia kwa ukali sana na kudai tumeibiwa sana katika awamu zilizopita. Kwamba yeye amekuja kuinyoosha nchi na kufagia ufisadi na mafisadi wote na kuhakikisha nchi inaendelea na inaweza hata kuwa donor country.

Alisimamisha haki nyingi za watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla hadi kazi ya kusafisha nchi ikamilike. Na alidai katoa maisha yake mhanga kupambana na mafisadi kwa ajili ya wanyonge wa nchi hii.

Duniani kote alijulikana kama “a no nonsense anti corruption, anti graft” president.

Bila shaka utaelewa, kwa nini watu wanashangaa kujua kuwa hata yeye alikuwa “mpigaji”. Labda isiwe kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…