Chipsi za kfc huwa zinakaangwaje? Mbona size moja na tamu mno

Chipsi za kfc huwa zinakaangwaje? Mbona size moja na tamu mno

Wadau naomba kufahamu kama kuna anaejua chips zile zinatengenezwaje sio kwa utamu ule.

Nataka kukaangaa mithili ya KFC ili niuze sana uswahilini

Shukran
Mkuu angalia process ya kutengeneza Frozen fries . Kikawaida KFC wananunua hivyo viazi kama sijakosea vinatoka Egpty kwa huku kwetu, kuna Mashine ina Menya then inakata halafu inachemsha ama kukaanga kidogo sana kama sekunde kadhaa kuua wadudu halafu vinaingia kwenye Freezer kugandishwa.

Kutoka hapo ndio vinauzwa sasa kwenye Makampuni kama KFC, Mc donald na wengineo.

Kuelewa Zaidi tembelea supermarket yoyote nenda upande wa MA fridge/freezer tafuta hizo frozen fries nunua halafu kakaange nyumbani.

Zipo kama hivi
images-9.jpeg

So utofauti na chips za kawaida mtaani ni huko kuchemsha kidogo na kuzigandisha kabla ya kuzikaanga.
 
Ingia YouTube, hata za McDonald zipo pia, viungo unaweza kuchanganya vya kwako zikatoka tamu zaidi, muhimu ni process kuanzia kukata, kuviloweka , aina ya viazi ,kukausha etc na wale kuku wao wanapikwa kwenye high pressure fryer ndio maana wako soft na crunchy
 
Kweli kabisa unachosema ila la kuongezea tu sisi tunajua viungo tulivyo navyo na tulivyozoea tu na hakuna wa kujiongeza
Kuna msomali nilimuona youtube jamaa kasoma nje kaamua kwenda kenya na kuchukua shamba kubwa na amelifanya la kumwagilia
Amepanda Celery, parsley, Dill, caraway, coriander na vingine nimesahau
Yaani kwa sasa anasafirisha uk na Germany
Sasa hata sisi tungevitambulisha nchini kwa wingi mpaka mama ntilie na mahotelini wakatumia nafikiri mapishi na ladha ingebadilika kabisa

Aise viungo vinabadili dish
Vikitumika hivyo viungo mtakubali kuuziwa wali nyama elfu tano badala ya elfu mbili mia tano?
 
Vikitumika hivyo viungo mtakubali kuuziwa wali nyama elfu tano badala ya elfu mbili mia tano?
Chips na fries tofauti yake ni ukataji tu
Chips ni kubwa na fries ni nyembamba hapo ndio kwenye utamu na viungo kiasi
Mkuu kuna restaurants za kawaida tu unakula kwa 15,000 wali nyama Dar
Kwa mama ntilie au baba lishe kama ni fries 🍟 na mishikaki mbona utatoa tu kama imetengenezwa vizuri na kuzingatia usafi
 
Umesema dar ila magu huo msosi wa elfu kumi tano utakula mwenyewe
 
Umesema dar ila magu huo msosi wa elfu kumi tano utakula mwenyewe
Ndio maana pakaitwa jiji, mji, kijiji nk
Huku nilipo kikombe cha latte ni £3.51 sawa na 12,600 ya bongo na hakuna za bei ya chini
Kila sehemu na maisha yake boss
Na huko Magu wanauza kutokana na vipato vyao pia
 
Secret recipe sio siri tena watu wanatoa siri sana ila sio viungo bali ni kiasi unachoweka
Sasa basi kwenye French fries za KFC zinapokatwa huwa wana changanya na Unga wa vitunguu na Unga wa carrots na celery pia butter halafu wanaweka kwenye freezer zigande
Baada ya hapo kabla ya ku.... jisomee Google kumalizia mapishi nimechoka
Vipi hali mkuu, ukipata wasaa tuwasiliane PM inshaallah kuna jambo unishauri, urgent.
 
Think outside the box. Kwani Pepsi si imeajiri wafanyakazi? Sasa kama watu wameajiriwa na pepsi unawezaje kusema ni siri?
Huwa hawapewi formula,wao wanatengeneza tu,ndio maana hata wapishi wa KFC hawawezi kupika nyumbani chips au kuku kama wa KFC,Japo Kuna watu wana recipes ambazo zina karibiana but sio sawasawa na KFC.. either izidi au ipungue ubora
 
Mkuu ngoja nikuambie kitu kimoja ,unajua dunia hii kila mtu ana play part yake, kuna watu wao nature yao ni mabosi, kuna wengine nature yao ni wafanyakazi tuu, n.k n.k. sasa mfanyakazi hata uumpe recipe zote za kfc na umuonyeshe kila kitu bado atabaki kufanya kazi tuu.

Kwani mkuu mimi na wewe si wote tumeenda shule? Kwanini mimi na wewe hatujawa wanafunzi bora Tz, wakati tulikuwa na masikio, macho na kila kitu chakutufanya tuwe wanafunzi bora, kama alivyokuwa mwanafunzi bora lakini tukashindwa kuwa ? Nini tatizo hapa??
 
Binafsi sizionagi utamu wowote.

Kuku wao pia sipendagi gołymi yao ya kuweka ngano sijui coating.

Afadhali formula ya McDonald.

McDonald naweza kula lakini hao jamaa hata ukinipa bure kula nitajifikiria.
 
Back
Top Bottom