Chochote kizuri nikimhusisha mama kinakufa

Chochote kizuri nikimhusisha mama kinakufa

Hataki ufanikiwe au Amezungukwa na Mikosi Huyo Mama. Kikubwa Acha Kumhusisha
 
Hizo ni associations tu
Embu angalia ni wapi una-mismanage mambo yako badala ya kutafuta mchawi ni nani!

Mara zote mchawi wa mambo ya Mtu ni mtu mwenyewe!
Hapo hujatuambia tabia zako zipoje!
Unaishi vipi na watu,
Personality yako ni ya namna gani?

Hebu jaribu kujitathimini wewe kwanza na siyo kuangalia nje, tena kwa Mtu wa aina hiyo.

Tabia ya Watu tulio wengi mambo yakituendea mlama tunatafuta visingizio Hada hii tabia ya Kuanza kuoanisha mambo—Associations- hii ni tabia ya Mind ya kila mtu lakini- Check within- Within you.
 
Pole sana ! Omba kwa ajili ya vita iliyopo ndani yenu kupitia mama Yako mzazi ! Mungu akuongoze zaidi ...akupe maarifa na hekima zaidi jinsi ya kuamuaa na kuhakikisha usimukwaze mama !! AU AKIJA SEHEMU YOYOTE SEMA MANENO HAYA KIMOYO MOYO "Mungu najua wewe unawajua wazuri wangu na wabaya wangu,Na vunja roho ya uharibifu kwa kile chocolate nilichokianzisha kwa jina la Yesu kristo Amen" .... Mkaribishe kwa Tabasamu lote ila Imani iweke kwa Muumba wako !!
Shida itaanza pale akitaka kuomba yupo maji haaa haaa
 
Kuna ule msemo unasema hakuna kama mama kila nikiutafakari naona kuna watu wana bahati sana,lkn kuna sisi wengine tunapitia machungu sana kwa mama zetu na inakuwa ni siri tu unaitunza moyoni bila kumwambia mtu yeyote!,yaani hadi inafika kipindi unajiuliza huyu ni mama yangu kweli!?
Mkuu mama yako amekufanyaje?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Namshukuru Mungu nimejenga nyumba na nilifanikiwa kwasababu niijenga kwa siri kubwa.

Chochote ninachofanya kizuri au cha kimaendeleo nikimjulisha tu mama kinakufa.

Iwe ni ajira, akinitembelea ofisini kama sijaachishwa kazi bila sababu basi kampuni itafilisika, ili mradi tu niharibikiwe.

Nikajizoazoa nikafungua mgahawa, alipokuja tu, kwa siku nikawa napata mteja mmoja au wawili au hawaji kabisa, nikashindwa ku run business kabisa hadi nikafunga.

Nilikima matikiti, yakaota vizuri sana, nikampeleka shamba kuona jitihada zangu, baada ya siku mbili tu, matikiti yote yakaibwa shambani usiku na hawakuacha hata moja.

Hajawahi kumpenda mtoto wangu hata mmoja, wala mzazi mwenzangu yoyote.

Mimi ni mzaliwa wake wa pili, licha ya kwamba kwa baba yangu ni mzaliwa wa kwanza.

Huyo kaka yangu ni teja, lakini ndio kipenzi chake, kazaliwa mwaka 1976 lakini hadi leo anakaa kwa mama, watoto wake wanasomeshwa shule nzuri.
We Kuna kitu unataka kusema kuhusu bi mkubwa wako, Ila unataka ututumie sisi kutamka.
 
nilimuaga maza naenda kufanya kazi mkoa X badala ya Y, na nikamuonya asimwambie mtu yoyote akasema "sawa."
siku mbili nyingi akawaambia wamama wenzake kanisani! 😆😆
😂😂😂😂😂
 
Namshukuru Mungu nimejenga nyumba na nilifanikiwa kwasababu niijenga kwa siri kubwa.

Chochote ninachofanya kizuri au cha kimaendeleo nikimjulisha tu mama kinakufa.

Iwe ni ajira, akinitembelea ofisini kama sijaachishwa kazi bila sababu basi kampuni itafilisika, ili mradi tu niharibikiwe.

Nikajizoazoa nikafungua mgahawa, alipokuja tu, kwa siku nikawa napata mteja mmoja au wawili au hawaji kabisa, nikashindwa ku run business kabisa hadi nikafunga.

Nilikima matikiti, yakaota vizuri sana, nikampeleka shamba kuona jitihada zangu, baada ya siku mbili tu, matikiti yote yakaibwa shambani usiku na hawakuacha hata moja.

Hajawahi kumpenda mtoto wangu hata mmoja, wala mzazi mwenzangu yoyote.

Mimi ni mzaliwa wake wa pili, licha ya kwamba kwa baba yangu ni mzaliwa wa kwanza.

Huyo kaka yangu ni teja, lakini ndio kipenzi chake, kazaliwa mwaka 1976 lakini hadi leo anakaa kwa mama, watoto wake wanasomeshwa shule nzuri.
Pole mkuu....

Nitafute tuyajenge.....
 
Back
Top Bottom