Chochote kizuri nikimhusisha mama kinakufa

Chochote kizuri nikimhusisha mama kinakufa

Yaani nimefuatilia tangu kipindi nasoma, siku nikimuambia tarehe ya mitihani huwa ananiambia ataniaombea, huo mtihani hata kama ni mrahisi lazima nifeli. Siku nisipomuambia nitafauli hata kama huo mtihani ni mgumu

Michongo mingi ya kitaa nikimshirikisha lazima iende tofauti.

Mwaka huu nimekuja kuhitimisha kwamba mawazo yangu ni sahihi baada ya kufanya jaribio hili; Nimemshirikisha kwamba nitaotesha alizeti ekari 2 kwenye shamba la nyumbani akaniunga mkono. Nikanunua mbegu ya alizeti inayotosha ekari 4 nikaotesha ekari mbili hapo nyumbani, then nikaotesha ekari 2 kwa siri kwenye shamba la kukodi hapo jirani na shamba letu. Cha ajabu ile ya shamba la nyumbani haikuota lakini ile niliyootesha kwa siri imeota yote na inaendeleanvizuri kabisa. Kumbuka haya mashamba yamekaribiana sana; jiografia ni moja na tabia ya nchi ni moja. Hapo ndipo ni kahakikisha kwamba mawazo yangu ya mda mrefu ni ya kweli.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Namshukuru Mungu nimejenga nyumba na nilifanikiwa kwasababu niijenga kwa siri kubwa.

Chochote ninachofanya kizuri au cha kimaendeleo nikimjulisha tu mama kinakufa.

Iwe ni ajira, akinitembelea ofisini kama sijaachishwa kazi bila sababu basi kampuni itafilisika, ili mradi tu niharibikiwe.

Nikajizoazoa nikafungua mgahawa, alipokuja tu, kwa siku nikawa napata mteja mmoja au wawili au hawaji kabisa, nikashindwa ku run business kabisa hadi nikafunga.

Nilikima matikiti, yakaota vizuri sana, nikampeleka shamba kuona jitihada zangu, baada ya siku mbili tu, matikiti yote yakaibwa shambani usiku na hawakuacha hata moja.

Hajawahi kumpenda mtoto wangu hata mmoja, wala mzazi mwenzangu yoyote.

Mimi ni mzaliwa wake wa pili, licha ya kwamba kwa baba yangu ni mzaliwa wa kwanza.

Huyo kaka yangu ni teja, lakini ndio kipenzi chake, kazaliwa mwaka 1976 lakini hadi leo anakaa kwa mama, watoto wake wanasomeshwa shule nzuri.
Mshukuru Mungu umejua, kuna watu wamebeba roho za mauti kwa kujua au bila wao kujua.
Roho za mauti huua mawazo mipango malengo yote ya mafanikio.
 
Inasemekana mama hutoa laana baba hutoa baraka, kwa hiyo hata iweje mama hawezi toa baraka ndio maana baba nae hawezi toa laana ipo hivyo
 
Hata kitu ukiwaambia marafiki au ndugu huwa hakifanikiwi sijui kwanin
Kuna wakt nilimshirikisha rfk angu San mshikaji wangu kuhusu kuanza ujenzi wa nyumba yangu Arusha kule na Ni yey peke ake nimemuambia uwezi amini sjijanga hyo nyumba mpk sas

Ajbu nadhani ndani ya week moja baadae aliambia na yey anataka kujenga ktk kiwanja chake alivhopewa na Bab ake kule Moro na alikuwa Hana Kaz yoyote ile Yuko nyumban tu ajabu hat yey pia hukujenga mpk sasa ingawa sas HV Ana kazi yake

Ukweli Ni kuwa mamb ya maendeleo haipazwi kutangazwa kwa watu iwe hat mke wakt mwingine mshirikishe
 
Mimi pia nina tatizo hili. Ni mwaka wa pili tangu nifahamu kwamba Kila ninachomshirikisha mama kinafeli. Kwa sasa najikusanya nihame mkoa kwa siri na kamwe sirudi hata nikisikia amefariki siji kumzika.

Nimejaribu ku Link dots hata huu umaskini unaotuandama unasababishwa na yeye.
Ahahahah
 
Mleta mada fanya kimya kimya kuna ulazima gani kumwambia kila kitu unachofanya wewe kwa faida yako,mkeo na wanao?
Kuna vijana wengine useless kila anachofanya lazima apige simu kwao kuwahadithia,yaani hata akijisaidia pembeni ya choo lazima wazazi/ndugu zake wajue.
Ndio mwanzo wa kupigwa vipapai na kuchukua magundu ya wengine.
 
Back
Top Bottom