Correlation is not causation.
Inawezekana mtambo wa maji ya line inayokuja kwako ukawa unaruhusu maji yaingie sumu kila Jumapili jioni, labda kuna mfanyakazi mzembe zamu yake ni Jumapili jioni hajui kuweka filter ya kuzuia sumu kuingia kwenye maji line ya mwisho kuingia kwako, na mama yako anakuja kukutembelea kila Jumapili jioni.
Ukaona kila Jumapili jioni mama yako akija kukutembelea watu wa nyumbani kwako wanaumwa, kwa kunywa maji yenye sumu.
Ukasema huyu mama yangu ni mchawi, kila Jumapili jioni akija, watu wanaumwa.
Kumbe ni mambo tofauti yanaendana, bila moja kuwa sababu ya jingine.
Ila, kwa tabia zetu za kukimbilia kuunganisha mambo kichawi, huyo mama haponi hapo.