Chonde chonde mnao-dislike nyuzi za watu - haya yatawapata!

Chonde chonde mnao-dislike nyuzi za watu - haya yatawapata!

Juz nilijikuta nimesinzia kisa haya magazeti😅
Noma sana. Nimekumbuka zama za Tanganyika Library, ile njuka wanajifaragua kiingereza wanakijua kwahiyo ili kuuza sura wakawa wanajifanya wanasoma The guardian na Daily News.
Yaani nusu saa nyingi wanapitiwa na usingizi, na ile migazeti ilivyo mikubwa wanakuwa kama wamejifunika mashuka yenye maandishi
 
Kumbe Hamna kitu🤣
 
Katika ulimwengu wetu wa kidijitali, chuki hujidhihirisha kwa njia ya matusi au kejeli, lakini pia hujificha kwenye emojis kama hizi: 😡😕 😠 👿

Watu wengine huonyesha chuki yao kimya kimya kwa kum-ignore mtoa mada.

Chuki inaathiri nafsi ya mtu na jamii kwa ujumla. Chuki ni sumu inayoharibu kidogo kidogo afya ya ubongo na moyo. Tafiti zimeonyesha kuwa mtu mwenye chuki ya mara kwa mara huwa na viwango vya juu vya cortisol (kichocheo cha msongo). Hii huathiri kumbukumbu, usingizi, na huongeza hatari ya magonjwa ya moyo.

Chuki huathiri hisia na tabia. Chuki inazaa hasira na kumfanya mtu ashindwe kutulia. Mtu mwenye chuki hutumia muda mwingi kufuatilia mtu wa kumuangusha badala ya kutafuta njia za kujiboresha yeye. Jambo hili linaweza kumchelewesha kifikra, kibiashara na hata kielimu.

Chuki inaweza kumfanya mtu ashindwe kujifunza kutoka kwa wengine. Hata ujumbe wenye hekima ukiletwa, mtu mwenye moyo wenye chuki hukataa kuupokea ujumbe huo kwa sababu anamchukia mtoa ujumbe.

Ku-dislike mada au uzi kwa emojis za chuki ni kama kusema: "sikubaliani na wewe," "natamani ushindwe."

Mbaya zaidi chuki huleta uharibifu wa kiroho. Hupunguza uwepo wa Mungu ndani ya moyo: Biblia inasema, "Yeye asemaye anampenda Mungu naye anamchukia ndugu yake ni mwongo" (1 Yohana 4:20). Huwezi kuwa karibu na Mungu kama unawachukia wengine, hata kama chuki yako ni ya kimya kimya. Na waongo, adhabu yao inajulikana. Ni kutupwa katika ziwa la moto, milele na milele (Ufunuo 21:8)

Ila mimi nikiwekewa emoji ya dislike, najua nimempiga shetani penye mshono. Shetani na maajenti wake, kamwe hawawezi kunipenda kwa sababu namulika nuru gizani. Shetani ananichukia kwa sababu namnyang'anya watu aliowafunga minyororo. Hivyo nikiwekewa emoji za ku-dislike nahesabu nimepewa kombe la ushindi 🏆💪😀
Ufu 3:21
Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi...
Hivi Tlaatlaah nyetoman 🐒 na mshamba wa shambwa, ni dam dam na Setfree
 
Watu 14 kati ya 23 wamedislaiki uzi wako... Hawa ndio wale wakipoteza hela barabarani wanaenda kupiga mke nyumbani 😄
 
Watu 14 kati ya 23 wamedislaiki uzi wako... Hawa ndio wale wakipoteza hela barabarani wanaenda kupiga mke nyumbani 😄
Hao ni wale walioshangilia niliposema "Kwaherini ndugu zangu wa JF" Sasa nimerudi nawamulikia tochi wanatafuta pa kujificha hawaoni; na shetani aliyewapofusha akili hapendi nuru kabisa. Hakuna jinsi itabidi ama waokoke au wakatae waende motoni. Nimeishasema: dislike kwangu ni kikombe cha ushindi. Nimempiga shetani "KO"
 
Haya, tema mate tuwachape
 
Back
Top Bottom