Chondechonde Maalim Seif Sharif Hamad

Yakhe uachaguzi sio vita atiii. Tujenge Nchi yetu maisha yaendelee. Usikae na kinyongo haya mambo yashaisha, inaelekea wewe hujui siasa ndio maana wapata shida shida sana. Eti nawewe una mshauri Maalim, hivi kati yako na yeye nani anajua vema siasa?. Kauze urojo na juice ya Miwa ulipe ada za wanao ulamaa
 
Exactly , Maalim Seif asikubali kabisa kushiriki serikali ya wamwaga damu .Yaani mimi sikujua kabisa kama CCM na viongozi wake wanashida na uongozi wa nchi sana kiasi cha kumwaga damu za maelfu ya watu ili tu wabaki madarakani .
Damu za maelfu zilimwagika wapi? Acha kuandika vitu ambavyo huna ushahidi navyo.
 
Naunga mkono hoja. Hatutaki ulaghai. Ajue watu wamekufa wakipigania yeye ashinde kihalali. Leo kaibiwa mchana kuzimu hakuna nyota. Asikubali. Umma uko pamoja naye.
 
azanzibari wameuliwa, wamejeruhiwa wamenyanyaswa na kupotezwa who cares? Mara ngapi yamefanyika mini kimepatikana
Haya ndio yanayojenga hoja ya Maalim akatae. Hivi akakae na wauaji wa watu wake kwa jina la kutaka uraisi na kejeli pamoja na jeuri kwamba serikali hatapewa Hizbu? Iwe kashiriki au vingonevyo, kuungana nao ni kuhalalisha mauaji.
Naunga mkono hoja ya Maalim Kutoshirikiana nao.
 
Kwa hiyo what next?

Pitia tena comment yangu.

Hasira bila mipango haziseidii.

Mbinu zote zimeshafanyika long time. Hazijasaidia
 
Kwa hiyo what next?

Pitia tena comment yangu.

Hasira bila mipango haziseidii.

Mbinu zote zimeshafanyika long time. Hazijasaidia
Sina njia mbadala zaidi ya kusisitiza Maalim asikae na wauaji wa kisiasa kwani ni aibu na fedheha kwa waungwana.
Maalim asikae na uongozi huu labda kwa majadiliano akiwa nje ya mfumo. Elewa: Kwa msimamo wa CCM haitatokea siku wakaacha udikteta wao kwani kwao kutawala ni by hook or crook.
 
walisema mungu apende asipende kwao ushindi ni lazima So ni vyema kuwaacha na ushindi wao mana hatujui kama mungu kapenda ama hakupenda bora wabakie wao tuu
 
Unasema hili ni Tangazo Rasmi kwani umelilipia? Kwani unafikiri ukijitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar mambo hayataenda? Mbona mwaka 2015 mlijitoa na mambo yalienda kama kawaida. Akili za kuambiwa changanya na zako mkuu!!
 
Mmeshapigwa mechi imeshaisha hiyo sasa tunaendelea kupiga kazi tu!
 
U
Unamshauri mtu ambae hana zaidi ya miaka mitano inatakiwa awe amakufa kupisha wengine wazaliwe?
Yaani akikataa hii mitano hana kitu kingine anaweza kuifanyia zanziba kwa umri wake.
Mdanganye afe bila sifa yoyote.
Je umepata kazi kwenye entry za kuzimu,unaweza ukafa wewe yeye akendelea kudunda mbona wapo wengi tu .tulia.
 
Nakubaliana na wewe mkuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo mnapiga kelele umu ndan kwa nguvu kubwa wakat mnapo itajika kujitoa nguvu zenu Hua hamuonekan

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kususia nini kifuate. Kama kuna guarantee ya haki kutendeka sawa. Nahofia kama ya 2015.

Katika mazingira hayo ndio nikasema bora waingie tu.

Unafiki was CCM unaendelea tu. Roho za wazanzibari zinazidi kupotea.

Tutulie kufanya tathmini. Jazba haina maana.

Mimi naamini katika kupunguza madhara na kuyafanya mapambano yadumu.

Sasa hivi kuna dhoruba LA kisiasa, linahitaji majemedari hodari kuusoma mchezo.

Narudia tena jazba haifai lazima uwe na focus. Kususia kutapoteza hata network ya ndani.

Walau kushiriki kutapunguza madhara ambayo naamini CCM wameshayapanga.

Hiyo GNU yenyewe inaenda kufutwa.

Itoshe tu. Maalim na ACT wawatafute wazee na kamati zao wajadili kwa kina na kupanga mikakati ya kuishi na adui na isiinekane usaliti.

Zanzibar iko pabaya sana. Nahodha hodari anahitajika sio jazba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…