Kumbuka kuna watu wako ndani na haijulikani mustakbali wao, kuna wale waliosafirishwa kupelekwa Tanganyika akina Mazuri Naibu Katibu wa ACT-Wazalendo lakini kuna wengine wengi Unguja na Pemba wanateswa kinyama, pia wewe hujui kinachoendelea kuna familia wamekimbia kusikojulikana kama pale Ngwachani Pemba kijiji kizima kimesambaratika kusikojulikana mateso kila aina kwa wapita njia eneo lile mpaka uonyeshe kitambulisho kama unakaa nje ya Ngwachani ndio unapita. Kule shumba Pemba karibu watu 60 wako ndani na mateso na kila siku polisi wanaenda kuangalia nani amerudi kijijini wanamshika zinaachwa nyumba za wana ccm tu.
Mimi nadhani maalim anaweza kukubali kwa masharti ili kunusuru zile familia ziwe huru na watu wengine ambao wanaumizwa kinyama. Kama watakubali kuwaacha huru ni bora kuliko hayo mengine watu watavumilia mpaka Mungu mwenyewe atakapoleta wepese juu ya hao madhalimu waliokubuhu.