Chongoleani, Tanga: Rais Magufuli na Museveni waweka la jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima - Tanga

hivi viongozi huwa hawapitii hivi vikundi kabla ili kujiridhisha na maudhui yanayowasilishwa? sasa hawa wazee wanaipiga kijembe Kenya live!
 
Huo wimbo uliomalizika hivi punde wa hao waliovaa kanzu ni wa kuichokoza Kenya kwa kuikejeli kuwa ilisema mradi hautafanikiwa. Hakukuwa na haja ya kuisuta Kenya hii ni kutaka kuleta choko choko zusizokuwa na msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mpaka nimeamua kuweka Tbc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni upuuzi tuu wala sijawaelewa..

Afu pia sikuona sababu ya kuvaa nguo za chama fulani..

Hili ni jambo la kimataifa..!
 
Hao wana kikundi cha burudani wajinga sana, sasa Kenya inausika vipi na uzinduzi wenu mpaka waitaje kwenye nyimbo yao
Hata mi nimeshangaa sana hao itaharibu sana uhusiano wetu na kenya
 
Hao wana kikundi cha burudani wajinga sana, sasa Kenya inausika vipi na uzinduzi wenu mpaka waitaje kwenye nyimbo yao
Mkuu alitaja Kenya uzinduzi daraja la Kigamboni. What do you expect? Rank and file follow the leader.
 
Nadhani mpaka waganda wanatucheka tunavyoshangilia utadhani mafuta yetu, kumbe njia tu kwetu
 
Reactions: Gut
Hata sionagi umuhimu wa hivi vikundi.. Ni ujinga ujinga tu!
 
Watanzania kama mlishindwa kufaidika na bomba lenu la gesi kutoka mtwara hili la mafuta kutoka uganda msitegemee kitu
Tujifunze kutafuta na positive angle kdogo! Mradi huu ungekwenda Kenya kama ilivyokuwa imepangwa awali mngekuja hapa na mzigo wa matusi kwa Serikali.

Leo Viongozi wetu wamejitahidi kushawishi mradi huu mkubwa wenye faida kubwa kwenye nyanja zote za kijamii tunabeza tena, hv ni lini tutaanza kuona kama hata makubwa kiasi hiki hatuoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mradi wa bil $ 3 nchi nzima imehamia tanga, siku acacia wakitulipa zile $ bil 190 zetu nadhani itabidi nchi nzima tufanye sherehe
 

Itakuwa wamelazishwa ,kwahiyo bora liende tofauti na clouds walioshikia bango kama ni bomba la Ruge vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…