Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
Acheni mawazo mfu, nguvu za Rais wa nchi yetu siyo za binafsi ni za kitaasisi na taasisi ya urais hajabadilika kwahiyo ebu tuache kujidhalilisha wenyewe. Rais hawezi kuwa na nguvu kama hana support ya watu wake na hii inamaana kuwa wewe mmoja unapoacha kum support Rais aliyepo madarakani, unakuwa msaliti kwa nchi yako kabla ya yule aliyesimama katika nafasi ya urais.
Tumuunge mkono Rais wetu pale ambapo tumeshaamua kama nchi, ndiyo maana ya ile kura uliyopiga ili kumpa ridhaa Rais kusimama kwaniaba ya nchi katika maamuzi na utendaji wa serikali ndani na nje ya nchi. Hii itaongeza morale na confidence yake katika kuisimamia nchi. Kinyume chake ni kuyumbisha umoja wa kitaifa na hatimaye sote tukiyumba hakuna anayebaki salama
Mtu yeyote muungwana ana nidhamu na ni mtii kwa mamlaka inayo mwongoza. Ukikosa utii basi tambua thamani yako haipo siyo kwako, familia au taifa unaloishi.
Nilichoandika na ulichoandika vina uhusiano gani? Are you barking up the wrong tree?