Mkuu nimeona nichangie kidogo kwenye comment yako ili kutoa faida kwa watumiaji wengine. Hoja yako kuhisi kuambukizana magonjwa ni hoja sahihi kabisaa! Lkn nilivyosoma michango mingi ya wachangiaji nadhani wengi kutokana mazoea tunaamini hayo ndo matumizi sahihi ya hivyo vyoo.
Mkuu zile toilet paper zinazowekwa chooni,huwa ni maalum kwa ajili ya kuweka hapo juu ili ukae kuepuka kuchangia makalio na wengine. Zile siyo za kuchambia km watumiaji wengine wanavyodhani.
Kumbuka vyoo vya aina hiyo vinahitaji maji ya kutosha kwa ajili ya watumiaji na kufanyia usafi. Na ndo maana maji ya kusafishia baada ya kujisaidia yamewekewa pressure kali sana ili kuondoa uchafu.
Kuhusu Yale maji yaliyoko pale kwenye shimo la sink,yale ndo yanakata harufu ya choo,hivyo lazima yawepo na hayaepukiki kwa choo cha aina hiyo. Lkn km ulivyosema hayo maji kweli ni machafu,na ukijisaidia kwa kulenga shimo automatically yatakurukia.
Kukaa na kulenga shimo ni kutokujua matumizi ya choo,kile choo kimewekwa slop unatakiwa kujisaidia huku juu kwenye mlima wa sink ile utakapo-flash maji yatazoa kile kinyesi kutoka huko mlimani kuteremsha chini kwenye shimo.
Unajua kwa nn mzungu aliamua kuweka ujisaidie huku juu,hii inasaidia kukiona kinyesi chako umejisaidia cha aina gani,pengine kimechanganyika na damu au rangi isiyo ya kawaida. Hii inakusaidia kuonana na madaktari kujua shida ni nini na ndo maana sink la choo linawekwa rangi nyeupe ili kurahisha kuona. Matumizi ya choo cha shimo huwezi kuona kinyesi chako km kinashida au la!
Sent using
Jamii Forums mobile app