KERO Responded Choo cha Wanafunzi Shule ya Msingi Lima, Wilaya ya Nyasa (Ruvuma) ni kibovu sana na kichafu

KERO Responded Choo cha Wanafunzi Shule ya Msingi Lima, Wilaya ya Nyasa (Ruvuma) ni kibovu sana na kichafu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wakati nakua ilikua vitu kama choo inatumika nguvu ya wananchi.
Nafikiri serikali inabidi kuwapa wananchi Elimu.

Ujenzi wa Vyoo
Ujenzi wa madarasa
Maboresho

Mambo yote haya wananchi wakishirikishwa wanaweza wakatoa mchango wao .

Just imagine Vyoo tu ambavyo havizidi 10M wanasubiri sisiemu uwajengee sisiemu ambayo imeshajikatia tamaa
 
Viongozi ni reflection ya sura ya wananchi. Yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba ukitaka kufanya tafiti yoyote kuhusu wananchi usitumie gharama kubwa. Wewe angalia viongozi wao, vivyo ndivyo walivyo wananchi wao.
Hapo mkuu wa shule amepiga kelele kwa mkurugenzi au afisa elimu anapigwa danadana tu

Karne hii mtoto wa primary anajisaidia kama mjusi.

Nchi ambayo ina maziwa makubwa zaidi ya 3, nchi ambayo ina bahari from north to south, nchi ambayo ina maelfu ya wachina wamesambaa Tanzania yote wanachimba madini.

Tunasubiri COVID-19 ilipuke ili tupate msaada wa vyoo.

Nchi ambayo matajiri ndani ya masaa 3 tu wanachanga mabilioni kwaajili ya chama cha siasa.

Miezi michache iliyopita Wizara ya Afya ilitangaza ongezeko la mlipuko wa COVID-19 kwa % nyingi kuliko miaka yote ilihali mtaani kuko shwari ili tu wapate pesa za msaada.
Wananchi wa Wilaya ya Nyasa , hatumdai Rais Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom