Uchaguzi 2020 Choppa ya CCM yatua Urambo tayari kwa kampeni nchi nzima, sasa ni mashambulizi kotekote!

Uchaguzi 2020 Choppa ya CCM yatua Urambo tayari kwa kampeni nchi nzima, sasa ni mashambulizi kotekote!

Si juzi tu mlisema anatumia gari ili asikie matatizo kiko wapi sasa?
 
Kwa mujibu wa Ayo tv ile Choppa ya CCM tayari imetua Urambi mkoani Tabora kwa ajili ya kutumika katika kampeni.

Sasa ni mashambulizi kutoka kila kona ardhini, angani na majini, Tundu Lissu lazima akae.

Maendeleo hayana vyama!


Nawasihi CCM warejee upya maamuzi ya Kutumia Chopa. Naona kama watapishana na Kura. Hizi Kampen za ardhini zinawafikia watu wengi zaidi kuliko Kampeni za Kutumia Chopa.
 
Mdahalo unaleta maendeleo ?
Haa haa haa. Kumbe we jamaa sio mzima. Inamana huelewi umuhimu wa mdahalo Hadi muda huu??

Kimsingi kupitia mdahalo ndio tutajua uwezo wa wagombea wetu katika kuleta hayo maendeleo. Mpigakura hatakiwi kuviziwa, anapaswa ampigie mtu Kura akiwa na uelewa wa kutosha juu ya uwezo wa mtu huyo anayegombea.
 
Ni kwanini hamtaki mdahalo?
Mdahalo kwa masuala yapi! Hayo ya kudharilishana?

Mgombea mmoja anawaeleza wapiga kura nini alichofanya katika kipindi walichompa ridhaa ya uongozi ili wampime kama anastahili kuongezewa muda. Pia anataja mapungufu ya utekelezaji na jinsi atavyokamilisha akiaminiwa tena.

Mgombea mwingine anakandia aliyoyafanya mgombea mwenzake kwa lugha ya kashfa. Haelezi yeye katika kipindi hicho pia alifanya nini ili wapiga kura wampime. Anashindwa kueleza akipewa ridhaa ya uongozi atawafanyia nini wapiga kura kuondokana na umaskini. Yeye anabwabwaja na nadharia ya maendeleo. Ananukuu falsafa ya Baba wa Taifa ya Uhuru na Maendeleo akisahau kuwa Baba wa Taifa ndiye alikuwa mwasisi wa maendeleo ya vitu (alinunua ndege, akajenga viwanda, akaanzisha mashirika ya umma, nk).

Hawa wagombea wawili kamwe hawawezi kufanya mdahalo kwa kuwa mmoja wao anaishi kinadharia.
 
Vipi matamasha mmeamua kuachana nayo? au wasanii wanatangulia site kwa mabasi!!
 
Je chadema wakishinda wataweza kujaza nafasi zote serikalini ukianzia wakurugenzi wa taasisi mbalimbali
 
Alafu mnafikiri wananchi hawaoni uonevu wenu??? Juzi mmekataza Chadema kutumia chopa leo nyie mnatumia!!!!

Kwa udhalimu wenu huu lazima watanzania wote wawanyime kura mwaka huu!!
Mkuu si mlete tu rubani wa chopa ambaye hajazidi miaka 65 maana mnanza kutuchosha kweli. Au na wao naye ni kibabu?
 
mdahalo wa kazi gani ? kwan ww huwez kutofautisha mavi na mkojo? we tulia uliwe wakishiba watatuachia tu
Mataga huwa hamna msimamo, hapo Jiwe akosema yuko tayari kwa mdahalo(Japo ni ndoto kwani uwezo wake anaujua) wote mtageuka kama nzi wa kijani

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Hata wakimleta CCM na serikali ya magufuli watatafuta sababu
Wamlete kwanza. Sheria ni msumeno. Kumbuka chopa za kampeni zinaruka kwenye umati wa watu. Hivi kibabu kikisizi kwenye mashine na kudondokea watu nani atawajibika kwa yote!
 
Haa haa haa. Kumbe we jamaa sio mzima. Inamana huelewi umuhimu wa mdahalo Hadi muda huu??

Kimsingi kupitia mdahalo ndio tutajua uwezo wa wagombea wetu katika kuleta hayo maendeleo. Mpigakura hatakiwi kuviziwa, anapaswa ampigie mtu Kura akiwa na uelewa wa kutosha juu ya uwezo wa mtu huyo anayegombea.
Hahahahaaaaaaaa ! 😁😁😁😁 ! Yaani wewe mkuu Loxodona sijui una shida gani jamani! Yaani nielewe uwezo wa mgombea wangu mara ngapi? Huyo wenu sitaki hata kumsikia akafanye mdahalo na mzee wa ubwabwa ! Wakwetu na tangible record ya utekelezaji wa ilani ta CCM
 
Back
Top Bottom