Christiano Ronaldo ndiye wa kwanza kupiga Tik tak Duniani?

Ni goli lake la kwanza la ticktack
Hakuwai kuweza japo alikuwa anajaribu
Sio kweli!! Ana magoli mengi tu ya tik-tak, lakini hili LA sasa lina umaalumu wake kama ifuatavyo: 1. Mpira ulikuwa juu sana yaani futi nane (mita tatu kasoro kidogo). Niambie nani aliyewahi kuthubutu kupiga tik-tak mpira uliiko juu hivyo. Aliyewahi kupiga tik-tak iliyo juu angalau ni Ibrahimovich (futi 6) kwenye mechi kati ya England na Sweden, naye alisifiwa sana.
2. Mpira ule ulikuwa unatembea kwa kasi kubwa maana ilikuwa ni krosi, kwa hiyo kuthubutu kuufanyia timing mpira huo inahitaji ufundi mkubwa. Hakuna aliyetegemea ndiyo maana hata golikipa hakutikisika akabaki anauchungulia tu mpira ukienda wavuni!
3. Dunia ilishangazwa kumwona gwiji wa mpira Zinedane Zidane akipigwa na butwaa akabaki anatikisa kidole na kichwa badala ya kushangilia goli! Utakubaliana nami kuwa gwiji kama yule kupigwa na butaa hakikuwa kitu cha kitoto! Si rahisi kufanya kitu cha kumduwaza Zizu!!!
Goli la maajabu LA Zinedane lilikuwa pia ni over head kick lakini mpira haukuwa juu sana na sifa take pekee ni kuwa alifunga kwa umbali wa nusu kiwanja!! Ni goli zuri sana!!
 
Nakubaliana na wewe kuwa CR7 ana jukumu moja tu la kufunga ndyo mana anavizia sana.. Tofauti na messi ambaye ana majukumu meng ikiwemo la kufunga.

Ndyo mana ukiangalia la liga top scorers, mfungaji wa madrid yuko mmoja tu, CR

Ila wa barca wako wengi
 
Nimemtazama Zinedane mwanzo mwisho na Gaucho mwanzo mwisho! Ninakiri kwa soka la kuburudisha Gaucho hana mfano wala mpinzani! Lakini kwa habari ya "bicycle kick" hajawahi kutokea mchezaji kuthubutu kupiga tik-tak mpira unaokwenda kwa kasi na uko urefu wa karibuni mita tatu (futi 8) kutoka ardhini. Wengi hupiga tik-tak mpira ukiwa futi 3-4 kutoka ardhini. Kwa vyovyote vile hakuna aliyewahi kujaribu kupiga tik-tak mpira ulio juu kupita urefu wake, maajabu yako hapo!! R7 ana urefu takriban futi 6 na mpira ulikuwa futi 8 juu!!! Ibrahimovich ana urefu wa futi 7 aliwahi kupiga tik-tak mpira ulioko futi 6. Hakuna tuk-tak aliyowahi kupiga Gaucho zaidi ya urefu wa futi 4!
 
Safi sana
 
Hapo ndio wataelewa tofauti ya hiyo tiktak na ukilinganisha na wengine
 
Hajawai kufunga ata moja
Fatilia kabla hujaongea
Sijaja kuropoka
Kama unabisha leta ushaidi
Youtube ipo
 
Ulishaona goli la shakir wa Stoke city la hvyo???
Ronaldo ni mrefu ko mpira kuwa kimo hicho ni kawaida tu
 
Umeongea chumvichumvi nyingi ili kumsifia tu ila lilikuwa la kawaida tu
 
Hajawai kufunga ata moja
Fatilia kabla hujaongea
Sijaja kuropoka
Kama unabisha leta ushaidi
Youtube ipo
R7 kesha piga tik-tak nyingi tu japo ya aina hiyo kwa maana ya mpira kuwa juu sana ilikuwa ni burudani Mpya duniani, ndiyo maana hata kocha wake Zinedane badala ya kufurahi kushangilia goli alibaki anazungusha kidole kichwani kwa kuduwaa!!!
 
Faunali ya UEFA mwaka Jana walipoipiga juve 4-1, juve goli lao walifungaje, simkubali huyu jamaa
 


Rooney, Ibracadabra n.k walishafunga goli kama hilo yakaonekana ya kawaida tu πŸ˜€πŸ˜€ kafunga jamaa yenu juzi limekuwa la maajabu kweli kweli πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Cheki goli la Diego Maradona limeenda shule bwana...
 
Mashabiki wa messi mnateseka sana na CR7.
 


Duhh nimecheka sana πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Yupi unamkubali zaidi! MESSI AU RONALDO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…