Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Ndoa kama wakristo mnavyodai ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke ili kuwa mwili mmoja. Hivyo huyo Shusho na mumewe walikuwa mwili mmoja na ndoto zake zilitakiwa ziwe ndio za huo mwili mmoja (ndoa).


Sasa kama ni mkristo anaetambua hilo basi kusema alimuacha mumewe kufukuzia ndoto zake ni utapeli wa hali ya juu huu.

Atupe sababu nyingine. Asitulaghai sisi wenye akili.
 
Asirudi kuanza kulialia..!!
Unapoolewa au unapoowa, kuna mambo utayaacha. Sasa yeye alitaka aendelee na mambo yake kama bachela..!!?? Atoe ujinga wake..!!!

Katika vitu vinayowashinda wanawake, baadhi ni hivi;

1. Umaarufu
Wengi wa wanawake maarufu ndoa zao zina shida sana. Huwa wakishakuwa maarufu wanaona ndoa ni utumwa. Anataka awe popote muda wowote. Hii inakwenda hadi namna anavyowalea watoto wake.

2. Fedha
Mwanaume, anaweza akaishi na mwanamke asiye na kitu kwa maisha yao yote, lakini kwa wanawake walio wengi mwenye hela kuishi na mwanaume asiye na kitu, ikizidi sana wiki..!!

3. Cheo
Kuwa na cheo nako baadhi ya wanawake wameshindwa kujizuia kuwanyanya waume zao kwa vyeo vyao.

Huyu umaarufu tu unamsumbua..!!
 
Hivi, akiwa kama mchungaji, ATAFUNGISHA NDOA?
 
Ni kweli Mkuu
 
Utafiti unaonesha Waimbaji wa kike mara nyingi ndoa zao either zina viraka au zimevunjika kabisa
1) Beatrice muhone
2)Rose Muhando
3)Bahati Bukuku
4)Martha Mwaipaja na sasa
5)Angel Bernad
6) Christina Shusho

Hii sio Coincidence kuna shida mahali.
 
Wanawake wenye ndoa wasiende kwenye hilo kaisa. Awe mchungaji wa single mothers atatoboa.
 
Malaki 2:16

"Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana"

Mithali 2

17 Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake.
18 Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu.

Rafiki wa ujana ni mke au mme wako

AGANO la MUNGU wake ni NDOA

1 wakolintho

7.10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

7.11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe

"wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe"✍️
 
Nimemsoma sana anaposema nitimize ndoto zangu yaan awe na kanisa lake....kweli siku ile watakuja wengi wakisema walifungua makanisa yao.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…