Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Hii ni kauli ya dada mwimbaji wa siku nyingi aitwae Christina Shusho, "Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia.

"Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake.

Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"
Jambo jema ni kwamba anapingana na andiko la Biblia Takatifu kitabu cha
Ufunuo wa Yohana 22
18. Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
19. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

Na kila mtu akitaka kumfuata Yesu anapaswa kuamini na kuyaishi yale yote yaliyoletwa kwetu.
 
Labda ilishawahi kutokea katika karne za mitume Waliokuwepo awali?au wapi kwenye biblia ametajwa nabii yeyote mwanamke?
(Acts 2:17)

Itakuwa siku ya mwisho asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na Wana wenu na Binti zenu watatabiri, na vijana wenu wataota maono, na wazee wenu wataota ndoto.

KANISA lolote lenye Roho mtakatifu, lazima ziwepo karma Tano kuu, Unabii ukiwemo,

Ikiwa unasali Kanisa hakuna karama ya unabii au maono, watu hawaoti ndoto za Mungu, Hana Kanisa Hilo, mnaabudu katika mwili, Si katika Roho mtakatifu.

Na karama hiyo ya unabii ni ndani ya Kanisa, Si Nabii mwanamke afungue Kanisa, HAPANA.

Ubarikiwe!!
 
Labda ilishawahi kutokea katika karne za mitume Waliokuwepo awali?au wapi kwenye biblia ametajwa nabii yeyote mwanamke?
KAMA SHIDA NI NABII MWANAMKE TU, WAPO.

1. LUKA 2:36 INASEMA; 36 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. 38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
2. MKE WA NABII ISAYA; Isaya 8:3 inasema; Ndipo nikamkaribia yule nabii wa kike, naye akapata mimba na baada ya muda akazaa mwana. Mungu sasa akaniambia: “Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi,

3. WAAMUZI 4:4-5 INASEMA; Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. 5 Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.

4. KITABU CHA KUTOKA 15:20 INASEMA; Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.

5. All in all, siku hizi za mwisho, Mungu aliahidi kumwaga roho yake kwa wanaume na wanawake pia. YOEL 2:28 INASEMA: Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
 
Kauli kama hizi siyo za kufumbia macho, hawa wanakuwa wanatumwa na hidden society kuharibu taasisi na jamii, hivyo ni wa kumkemea kwa njia zote.

Hakuna wito wa kuvunja Ndoa pia hakuna Mungu atakayekupa ndoto za kuvunja ndoa yako ili ukamtumikie huyo ni sheitwan bin ibirisi.
Kukemea ndio kufanyaje ndugu?
 
Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake.
Sawasawa
 
Yule alishajiunga kwenye chama chetu kile cha wajenzi na mwenzie..

Kwenye lile tamasha la wasafi ndo ilikuwa kuwatambulisha rasmi.
 
Huyo dada yupo sawa kabisa kwa sababu hata mwanzo kabisa dini iliingia kimchongo tu kwa hyo jambo la kimchongo lazima liwe kimchongo ,bado hamjaona mengi yanakuja.
 
Tuliambiwa mwishoni kutakuwa na ujuaji mwingi sana.
Walio andika biblia walijua kabisa ipo siku watu wataamka na kuujua ukweli ndio maana walijifanya kutabiri ili kondoo mkiona hilo mkae kikondoo mpka kufa kwenu.
 
Hii ni kauli ya dada mwimbaji wa siku nyingi aitwae Christina Shusho, "Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia.

"Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake.

Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"
Kaamua afanye umalaya kwa uhuru kwa kupitia mapato ya biashara ya kabisa lake, muacheni.
 
Ameongea ukweli. Nyie mamburula ndio hua mnadanganywa na hao wachungaji feki na kudangaamyana eti mwili mmoja
 
Ameongea ukweli. Nyie mamburula ndio hua mnadanganywa na hao wachungaji feki na kudangaamyana eti mwili mmoja
OK, sasa yeye kama mchungaji, ameachana na mume, nani anafanya naye tendo la ndoa? au hafanyi tena, na kama anafanya, haoni kama atakuwa anazini? au imani yake inafundishaje?
 
Back
Top Bottom