CHRISTMASS ni ya kina Pope Julius I au ni yetu sisi na Yesu wetu?

Je ni maagizo kwa mujibu wa maaandiko? Au ni matakwa yako binafs..?

#MaendeleoHayanaChama

Jibu maswali yangu kwanza maana ndipo lilipo jibu lako. Kama kuna andiko litoe wewe unaeona kubadili siku ama tarehe kumeainishwa kama dhambi ipi ama kuvunja sheria ipi

Nikifanya kama inavyofanywa au nikatenga siku maalumu ya kuadhimisha kifo au kuzaliwa kwa Kristu. Nikafanya sala, kufunga na kumkiri kiimani.

Je, ninapata athari gani kiroho kwa kubadilisha siku hata kama ingekuwepo
 
Hakuna kinachoweza kubadilika, wewe kesho kula pilau tu.
 
wakina papa ndo wa anzilishi wa uchafu wote huu wakuchafua maandiko.watu mpaka Leo.wanajua siku inaisha saa6 usiku.wametu aminisha mungu.ana mtoto.tumekubali ukiwauliza mungu alizaa na nani uyo mtoto.wana kwambia ni mambo ya kiroho zaidi.japo Mimi ni mkristo ila sikubali kwamba mungu ana mtoto.maana nikujitoa akili.mungu.anazaha..
 
Umemaliza kila kitu, ila kwa Mtu punguani mwenye asili ya ubishi atapingana nawewe
 
Yesu alikuagiza waumini wasome Biblia kwa njia ya simu? Aliagiza watu waingie ibadani na suti?

Halafu hebu fahamuni neno ''KUADHIMISHA'' hamtapata shida yote hii.
 
Wewe ni Mfuasi wa Mwamedi na kama wewe ni Mkristo basi ni Mkristo jina

Hakuna Mkristo sahihi asiyeamini katika TRINITY
 
Wewe ni Mfuasi wa Mwamedi na kama wewe ni Mkristo basi ni Mkristo jina

Hakuna Mkristo sahihi asiyeamini katika TRINITY
najua ukristo auna shida ila kuna wahuni wachache wali uchanganya na upagani ndani yake.ila ukristo walio kuwa wanafundisha wanafunzi wa yesu.ushaalibiwa ndo maana kwenye ukristo. kuna madhehebu mengi mengi ujue.kuna shida.
 
Kwanza, hii calendar tunayotumia(wanaiita gregory calendar nadhani) ilianza lini?
 
... hakuna mahali maandiko yanasema ifanywe kumbukumbu..pasaka tu ndiyo alisema ifanywe kumbukumbu..
Na hakuna anayelazimishwa kufanya kumbukumbu, kila mtu na imani yake. Kama unaona si sawa kukumbuka siku ya kuzaliwa mwokozi ila ni sawa kukumbuka kuzaliwa kwako, hakuna shida yoyote maana ni imani yako, na si jambo jema kumshangaa anayefanya kumbukumbu ya kuzaliwa mwokozi wake. Kama tungekuwa tunaelewa maana ya IMANI, hata huu uzi haungestahili kuanzishwa maana wanaoadhimisha kumbukumbu sio wa imani moja na mleta uzi na wafuasi wake

Yaani ni sawa na na mwana CCM kushangaa ACT Wazalendo kuwa na cheo cha Kiongozi wa Chama eti kwa kuwa hakipo CCM, wakati katiba yao ACT inawaelekeza kuwapo kwa cheo hicho
 
Kwanza hakuna Mkristu anayeandika kwa makosa mengi ya kiuandishi kama haya
 
tusherekeeni tu hizi sikukuu za wenzetu maana hamna namna🍾🍾🍾
visikukuu vyetu hivi saba saba sijui nane nane hakuna vibe kabisa
 

Haujiulizi, kama sababu ya madhehebu kujitoa katika Ukatoliki ilikuwa ni moja (common), ni kwa nini basi yaanzishwe mengi kwa sababu hiyo hiyo? Kama A amejitoa katika B kwa sababu fulani, kuna haja gani na C kujitoa katika B na kuanzisha dhehebu lake kwa sababu ile ile? Kwa nini asimfuate A kwa kuwa sababu yao ya kujitoa katika B ni ile ile?
 
Mtoa post ungetoa na ushauri pia.
Dhidi ya Yesu kutokuzaliwa njiti, usilazimishe kwani hata mimba yenyewe ilitungwa kwa uwezo wa Roho Mtakaktifu. (shangaa hili kwanza)
Na kama tarehe 25 ilikuwa ni sikukuu ya kipagani na badala yake imegeuzwa kuwa ni sikukuu ya wakristo kusherekea kuzaliwa kwa Yesu ubaya uko wapi?
Kule makanisani anatajwa Yesu Kristo hiyo miungu imefutika kabisa ni wewe tu ndio unaifufua kwa faida zako binafsi. Kusanyiko la wakristo limetamalaki.

Haujapata kusikia kuwa vilima vitasawazishwa na mabonde yatafukiwa?
Wana wa Nuru wakishindana na wana wa giza , wana wa Nuru hushinda , pengine ndiyo maana hiyo siku yako ya miungu ikafutiliwa mbali na badala yake ikawekwa Krismas.

Amen!
 
Mkuu kwa nini hukumzungumzia japo kidogo pope julius, una muda bado waweza hata kwenye comments
 
Ningependa kuchangia mada hii LAKINI nimesita baaada ya kuipitia yote na kuona uelewa wa mleta mada. Kitu mabacho nataka nimkumbushe mleta mada ni kuwa hata katika maandishi ya kwaida, majina siku zote yanaandikwa kwa herufi kubwa. Kwa mfano si sahihi katika lugha yoyote kuandika jina la mtu kwa herufi ndogo, huwezi kuandika kwa mfano john joseph au mohamedi n.k. Hivyo namshauri anapoandika majina yoyote ayaandike kwa herufi kubwa! Inapendeza.
 
Christmas is not a Biblical festival. Hii ni sikukuu kama siku nyingine za kihuni duniani, Ni kama siku ya kuwakumbuka ma kayaman wote
Mzee katika Ukristo hakuna sikukuu zinazoamriwa kibiblia. sikukuu zote zimetokana na maazimio ya waumini walioona ni vema kukumbuka ukweli fulani ya imani na kuikumbuka kwenye siku maalumu.
Hakuna amri kukumbuka siku ya kufufuka kwa Yesu (Pasaka) wala hakuna amri ya kukumbuka kufika kwa Roho Mtakatifu kwa watu wengi (Pentekoste) wala kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu (Krismasi).
Kwa Pasaka na Pentekoste hao waumini wa siku za kwnaza waliweza kutumia tarehe zilizotajwa katika Biblia kwa hiyo walipanga tarehe zilizofaa na taarifa (kwa ufahamu wao - maana kalenda zilibadilika hivyo kila tarehe ni ya kibinadamu).
Kuhusu Krismasi hakuna dokezo la tarehe, Hivyo waliteua siku kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu.
Ambako hakuna ubaya, maana katika Ukristo hakuna amri wala maagizo kutoka Mungu kuhusu tarehe fulani.

Ndugu Waislamu wengi wanapenda sikukuu ya Maulidi, ambayo pia si tarehe ya kuzaliwa ya Mtume bali sikukuu iliyoanzishwa karne kadhaa baadaye. Waislamu wengine wanaipinga wakidai si halali kuanzisha sherehe isiyoamriwa katika Qurani au sunna ya mtume mwenyewe.

Waingereza husheherekea Queens Birthday kwenye mwezi ulioteuliwa kwa sababu hali ya hewa inafaa zaidi kwa sherehe ya umma, si kwenye siku alikozaliwa.

Ubaya wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…