Chui aliyevamia makazi ya watu katika mtaa wa Usalama, Kata ya Mahina Jijini Mwanza na kujeruhi watu wanne, akiwemo mtoto wa miaka kumi, mwananchi mmoja na askari wawili wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyama Pori, amedhibitiwa na kuuawa kwa kupigwa risasi kufuatia operesheni iliyoendeshwa na askari wa Mamlaka ya Uhifadhi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Polisi pamoja na wananchi.Mwenyekiti wa mtaa huo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa wakati pindi wanapoona wanyama wakali kwenye maeneo yao, kwani inasemekana baadhi ya wananchi walimwona chui huyo kwa muda mrefu bila kutoa taarifa mpaka alipoleta madhara.
Kwamba kumeonekana na kuwawa kwa chui mkubwa hivi mjini Mwanza?!
Kwamba chui alijeruhi mtoto wa miaka 10 na askari kadhaa.
Chui kuonekana mjini? Chui huondoka na swala kg 50+, hadi juu ya miti. Wetu anajeruhi watu? Chui gani huyu?
"Chui huyu siyo chui wa kufugwa aliyezowea kuletewa nyama za ng'ombe kwenye zoo fulani huko?"
Hakuletwa huyu makusudi ku ondoa attention ya watu na hoja ya magesi ya Oryx au yale mengine? Au zile hoja zingine zikiwamo zile nzito nzito za kutoana roho?
Kwa mwendo huu siyo tujiandae kuona mengi, almaarufu ya Mussa?