Chuki binafsi ya Haji Manara kwa Shaffi Dauda inatokana na nini?

Tunaitaji ufafanuzi na ushahidi zaidi tujue kama Haji alikosea, nilivyoelewa Dauda alisema Simba ni Underdog kwenye kundi alilopangwa na Haji akapinga .Je alitumia lugha ya matusi? Ni kweli Simba ni underdog kwenye kundi alilopangwa, je kama Haji Manara alipinga kwa lengo tu la kujenga kujiamini(confidence) ya timu yake ya simba atakuwa amekosea ? Ushindi si uwanjani pekee ukivulugwa kisakolojia lazima upingwe nyingi tena wamepangwa na waarabu, kwa upande wangu naona Haji Manara kafanya kazi yake vizuri sana.
 
Haji hakujibu kwa hoja,ametoa majibu atalipa kusasi km unakumbuka aliwahi kutoa tuhuma shaffih aliomba kazi WCB..sasa hii ni ishu person sio mpira
Sent using Jamii Forums mobile app
 
z
huyo zuzu 10 akawe msemaji wa familiya yenu sio Simba. Simba inahitaji msemaji kama Manara, alaf Simba inaingia vitani kuwakilisha Taifa, unapoiita Underdog unastahili bakora, Shafii apigwe tu. Simba inatisha Afrika nzima unaiitaje Underdog?
 
itakuwa ni yale mambo yao ya mademu naona....
 
Nadhani majina ya hizi tittle zinawafanya wengi kuwa "WATU WA KUBWABWAJA TU aka KUSEMA CHOCHOTE" nadhani wangefanya kazi kama "MAAFISA HABARI WA TIMU" naona mambo ya UWEDI yangezingatiwa....nadhani mbali na Dismas Temu, kuna msemaji wa AZAM Ndg. Maganga
 
Ahahahahahahaha ahahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chukulia mfano.

Champions League Group A

Barcelona

Chelsea

Roma

Sampdoria.


Nani underdog hapo kwa muono wako?! Ni halali msemaji wa Sampdoria kumtolea povu mchambuzi eti kisa timu yake imeitwa underdog kwenye kundi husika.

Basi angalau tujaribu kumpinga kwa hoja. Let's try hivi...

Kundi la Simba liko hivi

Al Ahly

Vita Club

Js Soura

Simba


Em iruhusu akili yako ifanye kazi achana na hizi pigo za Yanga Daima Mbele Nyuma Mwiko na Simba Nguvu Moja, tuambie nani kibonde hapo?!!

Ni fahari utapopata mafanikio huku ukiwa umetoka kudhauriwa. Kuwa underdog sio tusi haimaanishi huwezi kufanya maajabu. Rejea case ya Leicester city.

Ukubali ukatae Haji manara ni sababu pia ya Simba kukamiwa kwenye mechi zake na hivi vitimu vidogo. Kisa ni nini? Mdomo. Jamaa anaropoka sana. Psg wanafanya usajili wa kufuru lakini uwezi sikia msemaji wao anajitapa kwa usajili huu hakuna timu ya kutufunga. Mara oh tunaweza chezesha vikosi viwili ndani ya Siku moja vikacheza mechi mbili tofauti.

Huyu Haji Manara ana matatizo sana weka unazi pembeni. Em tuambie..... Shafii ni mwandishi wa Habari pia, kama we ni mdau wa kabumbu unatambua fika kipindi cha usajili tetesi nyingi huwa zinaibuka huyu kuhusishwa hapa and the likes. Na inafika kipindi inaeditiwa picha ya mchezaji fulani kavaa jezi ya timu anayohusishwa nayo. Imeshakuwa kitu cha kawaida dunia nzima ila huyu bwana alimtolea povu sana Shafii kana kwamba jamaa ndo anamshawishi Niyonzima ajiunge na Azam.

Kila mtu anajua humu ndani mimi ni shabiki wa Yanga ila inapotokea mambo yanaenda sio naenda directly kabisa kwamba hapa tunachochora. Hatuwezi fika popote kama tutakuwa watu wa kuoneana aibu. Mtu akizingua tunamchana. Kwenye siasa tuogope bunduki na huku michezoni tuogope nini kuongea ukweli?!

Sisi mashabiki tutabaki kuwa mashabiki na yeye Manara inabidi abehave kama kiongozi. Mimi naweza nikasema Simba hachomoki kwa Nkana huku nikijua fika matokeo aliyopata ugenini yanambeba Simba zaidi ila nitaongea hivyo kwa kuwa tu mimi ni shabiki wa Yanga na nitaeleweka kwa Wanayanga wenzangu. Naficha uhalisia naongea uongo. Manara hatakiwi kuwa kama sisi.

Hakuna kitu nilifurahi pale Yanga kama kugoma kumrudisha Muro kwenye nafasi yake baada ya adhabu yake kwisha. Jamaa alikuwa anaichafua Yanga. Simba imeshaingia kwenye Kampuni sasa ni hatua kubwa sana ambayo hata mimi natamani club yangu ifike huko. Ila unapokuwa na msemaji ambaye hajui mipaka yake kuna siku mtakuja kulia na wadhamini. Rejea sakata la Mo kutekwa na post za Manara na kilochomkuta.


Anyway samahani kwa gazeti.
 
Umenena facts
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…