Prince Kunta
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 22,797
- 28,904
Duuh mkuu wa idara ndo anaandaa taarifa kama hiyo. Hivi H. Manara ana elimu kweli au kapata kazi kwa kimemoView attachment 981331
View attachment 981333
Sijamsikia akimkosoa January Makamba kwa hiki alichokosolewa, na ni wazi Manara ni Mweupe sana kichwani.
Sasa kilichokufanya na wewe umkosoe manara ni nini wakati na yeye ana mapungufu yake?Hata we unamapungufu km binadamu ,km dauda alivyokuwa na mapungufu...sasa kwann haji anataka kumzuia dauda hasifanye kazi yake km mchambuzi...?
Pia tambua kuna ukweli na kuponda unataka kuniambia simba sio underdog kwenye kundi lile?
Sent using Jamii Forums mobile app
Chukulia mfano.
Champions League Group A
Barcelona
Chelsea
Roma
Sampdoria.
Nani underdog hapo kwa muono wako?! Ni halali msemaji wa Sampdoria kumtolea povu mchambuzi eti kisa timu yake imeitwa underdog kwenye kundi husika.
Basi angalau tujaribu kumpinga kwa hoja. Let's try hivi...
Kundi la Simba liko hivi
Al Ahly
Vita Club
Js Soura
Simba
Em iruhusu akili yako ifanye kazi achana na hizi pigo za Yanga Daima Mbele Nyuma Mwiko na Simba Nguvu Moja, tuambie nani kibonde hapo?!!
Ni fahari utapopata mafanikio huku ukiwa umetoka kudhauriwa. Kuwa underdog sio tusi haimaanishi huwezi kufanya maajabu. Rejea case ya Leicester city.
Ukubali ukatae Haji manara ni sababu pia ya Simba kukamiwa kwenye mechi zake na hivi vitimu vidogo. Kisa ni nini? Mdomo. Jamaa anaropoka sana. Psg wanafanya usajili wa kufuru lakini uwezi sikia msemaji wao anajitapa kwa usajili huu hakuna timu ya kutufunga. Mara oh tunaweza chezesha vikosi viwili ndani ya Siku moja vikacheza mechi mbili tofauti.
Huyu Haji Manara ana matatizo sana weka unazi pembeni. Em tuambie..... Shafii ni mwandishi wa Habari pia, kama we ni mdau wa kabumbu unatambua fika kipindi cha usajili tetesi nyingi huwa zinaibuka huyu kuhusishwa hapa and the likes. Na inafika kipindi inaeditiwa picha ya mchezaji fulani kavaa jezi ya timu anayohusishwa nayo. Imeshakuwa kitu cha kawaida dunia nzima ila huyu bwana alimtolea povu sana Shafii kana kwamba jamaa ndo anamshawishi Niyonzima ajiunge na Azam.
Kila mtu anajua humu ndani mimi ni shabiki wa Yanga ila inapotokea mambo yanaenda sio naenda directly kabisa kwamba hapa tunachochora. Hatuwezi fika popote kama tutakuwa watu wa kuoneana aibu. Mtu akizingua tunamchana. Kwenye siasa tuogope bunduki na huku michezoni tuogope nini kuongea ukweli?!
Sisi mashabiki tutabaki kuwa mashabiki na yeye Manara inabidi abehave kama kiongozi. Mimi naweza nikasema Simba hachomoki kwa Nkana huku nikijua fika matokeo aliyopata ugenini yanambeba Simba zaidi ila nitaongea hivyo kwa kuwa tu mimi ni shabiki wa Yanga na nitaeleweka kwa Wanayanga wenzangu. Naficha uhalisia naongea uongo. Manara hatakiwi kuwa kama sisi.
Hakuna kitu nilifurahi pale Yanga kama kugoma kumrudisha Muro kwenye nafasi yake baada ya adhabu yake kwisha. Jamaa alikuwa anaichafua Yanga. Simba imeshaingia kwenye Kampuni sasa ni hatua kubwa sana ambayo hata mimi natamani club yangu ifike huko. Ila unapokuwa na msemaji ambaye hajui mipaka yake kuna siku mtakuja kulia na wadhamini. Rejea sakata la Mo kutekwa na post za Manara na kilochomkuta.
Anyway samahani kwa gazeti.
Yanga hatuna na haijawahi kuwa na shabiki anaeitwa shaffih dauda
HAMNA ww yule mtangazaji na mwenzie wa kituo kimoja cha kazi wanapenda sanaaa kuiponda SIMBA SC kila zuri simba wanalofanya wale mabwana wao kwao BAYA mimi namshauri huyo bwana mchambuzi wa kandanda AKAANZISHE CLUB YAKE ALAFU NDIO AIKOSOE KOSOE KILA ANAPOJISIKIA wala hakutakuwa na mtu wa kumpangia na kumzuia ila pale SIMBA SC watu wame weka PESA zao NYINGI tu sio kapesa kakuendesha tuvimichuano vya MANDONDO PESA iliyowekwa SIMBA inafungua redio kama anayofanyia kazi yy zisizopungua 5 tena classic studios Hivyo bac WATU pale SIMBA sc wapo MAKINI kila kunapo kucha kuna watu wana umiza AKILI zao juu ya iyo michuano sio kuimba konjera za kukosoa MBONA hakosoi YANGA ambao mpaka leo hawaja fanya uchaguzi licha ya serikali kuwaambia wafanye uchaguzi
Wanaosema manara ana chuki binafsi hawajalifuatilia ili suala wao wanaangalia instagram them wanakuja kuyaleta hapa. Wangekuwa wanasikiliza sports extra kuanzia simba inajiandaa kucheza na mbambane hadi juzi na nkana. Tena kabla ya mechi ya nkana shafii na geoff wakasema hawaoni jinsi simba itamfunga nkana taifa. Nikiangalia na kinachoendelea sasa, naona acha manara awatolee uvivu tu.
KWELI kabisa huyo GEOF utazani yy ndio mwamuzi MIMI nina amini hawa jamaa mwaka huu ndio mwaka wao wa kuumbuka LIVE mchana kweupeeee yaani geof yy ndio huwa ana conclude kabisaa eti juzi wale AL hilaly wamemsajili mchezaji toka CLUB cha EPL bac yy ndio akapata la kusemea , anasahau kuwa ktk mpira anything can happenWanaosema manara ana chuki binafsi hawajalifuatilia ili suala wao wanaangalia instagram them wanakuja kuyaleta hapa. Wangekuwa wanasikiliza sports extra kuanzia simba inajiandaa kucheza na mbambane hadi juzi na nkana. Tena kabla ya mechi ya nkana shafii na geoff wakasema hawaoni jinsi simba itamfunga nkana taifa. Nikiangalia na kinachoendelea sasa, naona acha manara awatolee uvivu tu.
Clouds pekee ndio walichambua hivo? Au kwa vile unasikiliza clouds tu? Redio kibao walisema hivo hivo na wanasema simba ni underdog mbona mapovu hayamtoki?
Pia umesema jef kahusika mbona anamwandama dauda tu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Uhuru/efm/ufm/radio1/magicfm/ nyingi tuRadio gani? Toa mfano. Haya nakuuliza na wewe, how simba ni underdog kwa Js Soura? Nijibu japo kwa statistics.
Clouds pekee ndio walichambua hivo? Au kwa vile unasikiliza clouds tu? Redio kibao walisema hivo hivo na wanasema simba ni underdog mbona mapovu hayamtoki?
Pia umesema jef kahusika mbona anamwandama dauda tu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kama hicho, nimewahi kumsikia oscar oscar baada ya mechi ya Nkana akielezea madhaifu ya simba kwenye difence na akaonya kuwa inaweza kutucost kwenye marudiano. Huyo ndio mchambuzi anakosoa na anatoa solution, sasa huyo naweza kumuweka kundi moja na shafii? Ambaye anasema simba ni undorg, hawezi fanya kitu kwenye kundi, how? Wana mapungufu gani? Warekebishe eneo gani? Hauwezi kusikia hilo kwa hao watu, wao kazi yao ni kubashiri tu.
Wewe utakuwa mbutembute fcUnaweza kuniuliza kwanini nasema chuki binafsi, Haji hataki Dauda aikosoe Simba kwa namna yoyote ile
Wachambuzi wengi wanatoa maoni yao juu ya Simba na Haji asemi chochote ila kwa Dauda ni ugomvi
Licha ya mapungufu ambayo Shaffi anayo ni ubinadamu tu, Haji huwezi kumzuia kutoa maoni yake kama mchambuzi. Hata yeye Haji uwa anakosoa na anatoa maoni yake mara nyingi tena kwa kejeli
Kwann Dauda tu? Huwezi kuzuia ukweli Simba ni underdog katika kundi lao huo ndio ukweli. Je, unataka usisemwe?
Shida ya Haji ni jeuri, kiburi, majivuno na ujuaji mwingi ili lazima akubali na anatakiwa kujirekebisha, ukimsikiliza wakati anahojiwa na media huwa anajibu kijeuri sana. Mbaya zaidi ajijui kama anamatatizo hayo niliyotaja..
Najua unapita JF au wapambe wako acha kujifanya TFF. Simba ni club ya Wananchi umeikuta na utaiacha, acha watu watoe maoni yao bila kuvunja sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jirekebishe....
Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikuwa sina mpango wa kukomenti hapa,ila jibu hili linafaa sana kwa mwanzisha uzi na wengineo "mbutembute fc"Tunaitaji ufafanuzi na ushahidi zaidi tujue kama Haji alikosea, nilivyoelewa Dauda alisema Simba ni Underdog kwenye kundi alilopangwa na Haji akapinga .Je alitumia lugha ya matusi? Ni kweli Simba ni underdog kwenye kundi alilopangwa, je kama Haji Manara alipinga kwa lengo tu la kujenga kujiamini(confidence) ya timu yake ya simba atakuwa amekosea ? Ushindi si uwanjani ukivulugwa kisakolojia lazima upingwe nyingi tena wamepangwa na waarabu, kwa upande wangu naona Haji Manara kafanya kazi yake vizuri sana.