hivi unawajua wachambuzi wa mpira?Yote kwa yote unadhani ni sahihi haji kumzuia dauda kufanya kazi yake km mchambuzi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Nakuunga mkono shafii ni bogas Amuige mwenzie Edo KumwembeUchambuzi gani wa kuikatisha tamaa Simba kila kukicha ? Kilasiku kilasiku Simba mbovu Simba vibonde.
Atoe basi hata pongezi kwa kuifikia hiyo hatua. Mchambuzi akitoa maoni, anatoa na mbinu ya kuweza kuuondoa huo ubovu anaouona kama wenzake wanavyofanya.
Aseme basi ubovu wa Simba uko wapi na urekebishwe vipi. Na sio kila kukicha ukiona anaizungumzia Simba basi kauli ni mbovu mbovu mbovu, vibonde,vibonde vibonde kila siku za uchambuzi.
Huu ni uchambuzi au udhalilishaji ?
Huu ni ukatishanaji tamaa. Aseme basi anataka Simba ijitoe ktk hayo mashindano au vipi ?
Mbona maneno ya kejeri kila kukicha ?
Huu sio uchambuzi ni ubabaishaji wenye nia ovu ya kuikatisha tamaa timu.
Wachambuzi ni akina Ally Mayai na Mwalimu kashasha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani akiita underdog ni tatizo! Au ni tusi? Ni vema wakiiona hivyo ili wasijiandae vya kutosha baadae wanapokutana Simba iwaonyeshe kazi kuliko kuonekana mabingwa na jamaa wakaingia kwa nguvu zote ikawa aibu nyumbani na Ugenini.Swali kama mchambuzi kwanini unachambua kwa upendeleo yanga huyu bwana hajawahi kuiponda lakin simba anaiita underdog huuu niujinga wa kupindukia
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tuache ushabiki tuje kweny ukweli japo huwa mchungu uliyosema ni kweli 100%√√√ manara anatuponza sana Simba na hana tofaut na Masau bwile nae anaiponza timu yake ukiongea maneno mbovumbovu ya kujiamini sana kuwa lazima nitamfunga mshindani wangu nae anajipanga ili kuficha aibu na. Kutaka kukata kauli zako hata kama hana faida na matokeo ushindi ktk ule mchezo ila kwa matusi yako na namna ulivojigamba aanaamua kukuzia kwani ni uongo mara ngap tunaona simba tunacheza na vitimu vya kawaida na vinatukamia na mwisho wa siku tunaaibika kwa kichapo kama sio suhuru nk... Manara ajitathimini kwa mwendo wake huo hatufai abadilike la sivo apige chini anajisifu sana acha majisifu fanya v oh vizur watu wakusifie sio ujisifu wewe no narudia tena kama manara hatabadilika na akaachwa aendelee kuwa msemaji wa simba tutakuwa na wakat mgumu sana kuwahi kutokea.. Pamoja na kuwa na hera pia na kikosi kizuri yangu ni hayo tu.. Nampenda msemaji wa yanga au azam akihojiwa anavojibu hadi raha lakini huyu. Mwite wetu ni shida ki2 kidogo tu mijisifa kibao mpaka anaharibu kama sio kuboa.. Ni kweli ktk michuano hiyo ya club bingwa afrka sisi simba ni underdog kwan kuna ubishi hapo ila tu mpira unadunda na mwamzi ni dakika 90 ila ukweli lazima usemwe kama ulivo.. Otherwise time will tell.Chukulia mfano.
Champions League Group A
Barcelona
Chelsea
Roma
Sampdoria.
Nani underdog hapo kwa muono wako?! Ni halali msemaji wa Sampdoria kumtolea povu mchambuzi eti kisa timu yake imeitwa underdog kwenye kundi husika.
Basi angalau tujaribu kumpinga kwa hoja. Let's try hivi...
Kundi la Simba liko hivi
Al Ahly
Vita Club
Js Soura
Simba
Em iruhusu akili yako ifanye kazi achana na hizi pigo za Yanga Daima Mbele Nyuma Mwiko na Simba Nguvu Moja, tuambie nani kibonde hapo?!!
Ni fahari utapopata mafanikio huku ukiwa umetoka kudhauriwa. Kuwa underdog sio tusi haimaanishi huwezi kufanya maajabu. Rejea case ya Leicester city.
Ukubali ukatae Haji manara ni sababu pia ya Simba kukamiwa kwenye mechi zake na hivi vitimu vidogo. Kisa ni nini? Mdomo. Jamaa anaropoka sana. Psg wanafanya usajili wa kufuru lakini uwezi sikia msemaji wao anajitapa kwa usajili huu hakuna timu ya kutufunga. Mara oh tunaweza chezesha vikosi viwili ndani ya Siku moja vikacheza mechi mbili tofauti.
Huyu Haji Manara ana matatizo sana weka unazi pembeni. Em tuambie..... Shafii ni mwandishi wa Habari pia, kama we ni mdau wa kabumbu unatambua fika kipindi cha usajili tetesi nyingi huwa zinaibuka huyu kuhusishwa hapa and the likes. Na inafika kipindi inaeditiwa picha ya mchezaji fulani kavaa jezi ya timu anayohusishwa nayo. Imeshakuwa kitu cha kawaida dunia nzima ila huyu bwana alimtolea povu sana Shafii kana kwamba jamaa ndo anamshawishi Niyonzima ajiunge na Azam.
Kila mtu anajua humu ndani mimi ni shabiki wa Yanga ila inapotokea mambo yanaenda sio naenda directly kabisa kwamba hapa tunachochora. Hatuwezi fika popote kama tutakuwa watu wa kuoneana aibu. Mtu akizingua tunamchana. Kwenye siasa tuogope bunduki na huku michezoni tuogope nini kuongea ukweli?!
Sisi mashabiki tutabaki kuwa mashabiki na yeye Manara inabidi abehave kama kiongozi. Mimi naweza nikasema Simba hachomoki kwa Nkana huku nikijua fika matokeo aliyopata ugenini yanambeba Simba zaidi ila nitaongea hivyo kwa kuwa tu mimi ni shabiki wa Yanga na nitaeleweka kwa Wanayanga wenzangu. Naficha uhalisia naongea uongo. Manara hatakiwi kuwa kama sisi.
Hakuna kitu nilifurahi pale Yanga kama kugoma kumrudisha Muro kwenye nafasi yake baada ya adhabu yake kwisha. Jamaa alikuwa anaichafua Yanga. Simba imeshaingia kwenye Kampuni sasa ni hatua kubwa sana ambayo hata mimi natamani club yangu ifike huko. Ila unapokuwa na msemaji ambaye hajui mipaka yake kuna siku mtakuja kulia na wadhamini. Rejea sakata la Mo kutekwa na post za Manara na kilochomkuta.
Anyway samahani kwa gazeti.
Mtazamo wangu, Haji kuitetea simba ni haki yake. Tatizo kwa Dauda, yeye ni mtangazaji na inatakiwa asionyeshe ushabiki wake umeegemea wapi wakati anachambua mambo ya vilabu.
Binafsi huwa simsikilizi Dauda maana huwa anajenga hoja za kukosoa tu na kuponda hata pale panapohitaji pongezi. Mbaya zaidi anatumia hisia za ushabiki wake binafsi na sio facts za kiuchambuzi.
Mfano uchambuzi wake wa juzi baada ya simba kuitoa khana, jamaa kakomalia kuhusu mafanikio ya yanga badala walau kuipongeza simba.
Pia ukimsikiliza hata kwa timu za ulaya, ni mnazi anaeipinga Man United waziwazi kwa hisia zake na sio facts.
Sent using Jamii Forums mobile app
Alafu mswahili ukimuuliza how simba ni underdog kwa Js Soura atakwambia Js Soura ni waarabu.
Huyo Haji ana tatizo zaidi ya hilo.Unaweza kuniuliza kwanini nasema chuki binafsi, Haji hataki Dauda aikosoe Simba kwa namna yoyote ile
Wachambuzi wengi wanatoa maoni yao juu ya Simba na Haji asemi chochote ila kwa Dauda ni ugomvi
Licha ya mapungufu ambayo Shaffi anayo ni ubinadamu tu, Haji huwezi kumzuia kutoa maoni yake kama mchambuzi. Hata yeye Haji uwa anakosoa na anatoa maoni yake mara nyingi tena kwa kejeli
Kwann Dauda tu? Huwezi kuzuia ukweli Simba ni underdog katika kundi lao huo ndio ukweli. Je, unataka usisemwe?
Shida ya Haji ni jeuri, kiburi, majivuno na ujuaji mwingi ili lazima akubali na anatakiwa kujirekebisha, ukimsikiliza wakati anahojiwa na media huwa anajibu kijeuri sana. Mbaya zaidi ajijui kama anamatatizo hayo niliyotaja..
Najua unapita JF au wapambe wako acha kujifanya TFF. Simba ni club ya Wananchi umeikuta na utaiacha, acha watu watoe maoni yao bila kuvunja sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jirekebishe....
Sent using Jamii Forums mobile app