Chuki dhidi ya January Makamba inatoka wapi?

We umetumwa, hao uliowataja ndio presidential materials,
 
Rais ajaye. Akili nyingi. Sasa hivi yuko Foreign Affairs kuwapa Watanzania heshima yenu..




Mengine yote majungu. Chadema hamumtaki mnajua atawakaza huko mbele. Watu wa Jiwe mna bifu nae kwa sababu ndio alimweka malaika wenu madarakani.


Mwengine nani Kigogo, anatukana ili apewe ela atulie.


Piga Kazi Kissinger Makamba
 
Hakuna chuki,uwezo wake mdogo,mbereko ndio kinga yake
 
Nahis ana Dharau, ubinafsi, unafiki na majivuno. Watu hawezi kukuchukia tu bila sababu, kuna vijana wanajiona wao ndiyo wao na hakuna wengine zaidi yao.
 
Rais ajaye wa kwenye familia yenu, majizi wakubwa nyie
 
Sukuma gang hao. Achana nao. Bado wanaomboleza
 
Chawa
 
Thibitisha kama anafaa + mgao wa umeme unaoendelea licha ya kutengewa bajeti kubwa ya matengenezo.
Pia ukipata nafasi tuwekee ushahidi wa hizo chuki dhidi yake na namna anavyofanya kazi Kwa matokeo chanya Kwa kila hatua zake.
Bila hata kuangalia ufanisi wake lakini jamaa ni wa hovyo kweli kweli. Kwanza anautafuta urais kwa uchu mkubwa halafu hakuna chochote ambacho amewahi kufanya kuonyesha kuwa ana uwezo. Fisadi mkubwa huyu. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hawezi kuchukiwa na wengi bila sababu.
 
Mengi tu ikiwemo kukomesha matumizi ya mifuko ya Plastics nchini jambo ambalo ni la kihistoria na lilikuwa mzigo kwa Taifa.
Sikiliza bro, Mkataba wa LNG kuanzia zero mpaka sasa hivi wanasign nani Waziri wa Nishati? FDI ya $40Billion haijawahi kutokea nchi hii.


Ukiwasililiza watu humu utafikiri Makamba hajafanya kitu.

Tanesco makes sense business wise now. Unaweza kupeleka mahesabu yake NYSE na ikawa listed. Lakini juhudi za Maharage wachumba chumvi hawazioni.

Sasa hivi hii nchi ina SHERIA ya Nishati safi ya kupikia. Mabadiliko ya tabia nchi tutaokoa miti mingapi tukiachana na kuni? Ila ooh Makamba hafanyi kitu.

Transmission lines kilometa ngapi zimejengwa wakati wa Makamba vs Waziri yoyote wa Nishati.

Pound to pound January kihistoria atakuja kuwa Waziri bora wa Nishati nchi hii haijapata kutokea.



Nimekaa paleeeeeeee.
 
Urais anautafuta au nyie wachimba chumvi ndio mnamtaja kwenye urais. Waliogombea 2015 wote kuanzia Mpina hadi Mwigulu mbona hamuwataji.

Na anautakaje kwa mfano, tupe evidence za yeye kuwa na uchu na urais.
 
Sijawahi kumkubali Huyo January makamba hata siku moja na sina alama ya kusimulia kuhusu uongozi wake zaidi ya nafasi yake kupwaya kwenye Kila WIZARA anayopewa. Kwa ufupi ni kiongozi anayewekwa kwasababu tu ya wakubwa kumwonea aibu kutokana na historical background ya familia yake. The same same to Riz1 kikwete, Nape, mwana FA, na wengine wa nafas ndogondogo za ukuu wa wilaya kama Good luck Mlinga na wengine wengi. Hawana uwezo wa Kiuongozi ila family background zinawabeba.

Kuna watu wamezaliwa kwenye familia ambazo historia zao haziwabebi kisiasa Wala Kiuchumi lakini Wana uwezo mkubwa sana wa Uongozi kiasi kwamba akipewa eneo la uongozi ndani ya mwaka mmoja tu watu wanashuhudia mabadiliko makubwa waliyodhani hayatatokea. That's all I can say.
 
Kumbe kahongwa na mtu binafsi? Nikadhani amekula Hela ya umma maana tumeambiwa ni fisadi wa Mali za umma nikadhani Kuna wizi kafanya!!
 
Kama tatizo ni CCM, hao uliowataja wako ndani ya kagenge flani kadogo(watu wacheche) ambao ndio wanaiendesha CCM Tena Kwa kutaka iendelee hivi hivi(kukumbatia kujuana,rushwa,ufisadi,kutokuwajibika,kutokufuta katiba na Sheria za nchi, incompetence serikalini, umasikini mkubwa Kwa watz, miradi isiyoendana na dhamani ya hela, name any)
 
Sio chuki mkuu.
Huyu ni kwa kuwa anajiinua hata ktk mambo ambayo tunajua wazi kuwa hana uwezo nayo hata kdg!
Uwezo wake ni mdogo sana kama wa Ridhawani.
Heis not creative at all, kama mnabisha tuambieni amewahi kufanya lipi jipya huko alikopita zaidi ya kutafuta hela kwa
mbinu zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…