Chuki dhidi ya January Makamba inatoka wapi?

January ni miongoni mwa viongozi bora sana tulionao kama nchi. Makelele unayosikia dhidi yake, ambayo haya ushahidi, ni kutoka kwa wasaka urais (wa baadae) ambao wanamuona tishio.

Pia, mimi naamini makelele hayo (hasa mitandaoni) ni moja ya mikakati wa baadhi ya vyama vya upinzani kushambulia vijana (viongozi watarajiwa) wa chama tawala, kama njia ya kuimarisha mbio zao za kusaka kushika dola. Inaonekana kama vile vijana wowote wa chama tawala wenye muelekea wa kuwa viongozi wakuu hapo baadae (January, Mwigulu, Kitila, Nape n.k.), lazima wasakamwe na kuchafuliwa hata bila ushahidi wala hoja za msingi.
 
Binafsi simchukii, sema January bila lile jina la Makamba basi angekuwa muosha Magari au kinyozi. Mwanangu huwa ananiambia hizi kazi hazihitaji kabisa uwe intelligent.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
January Makamba, mtoto wa Katibu Mkuu mstaafu wa CCM amekuwa akiandamwa katika mitandao mingi ya kijamii na kujaribu kuaminisha umma ya kuwa ni mtu hafai katika uongozi.

Binafsi Makamba nilimuona wakati wa utawala wa Kikwete akiwa ni mmoja wapo wa wasaidizi wa Rais Kikwete.

Mwenye ushahidi wa wazi kuhusu mabaya yake atuwekee hapa ingawa mimi namuona ni mtu humble, focused na mwenye uvumilivu.
Mazuri yake ni yapi??
 
January yupo kwenye Vita tangu aingie 5 bora Urais 2015.

Anaonekana ni threats kwa wenzake kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Ujao.

Wapo wanaotoa hoja kuwa hana Uwezo wa kuongoza ndiyo maana Wizara kadhaa alizoziongoza zimemshinda.

Kitu ambacho hawajui kuwa, Urais wa Tanzania sio kazi ya kubeba Zege kwamba inahitaji Ubaunsa.

Rais ni Taasisi, ndani ya Urais kuna Mainjini, Madaktari, Wanasheria, Maafisa Mipango, Wachumi n.k
Ni suala la mifumo kuachwa kufanya kazi.

Then yeye anachotakiwa kuwa nacho ni Ujasiri tu wa kufanya maamuzi kama alivyokuwa Ben Mkapa ama JPM lakini kwa kufuata Sheria na Katiba ya Nchi.

Hata mwenye Kidato cha Nne anaweza kuongoza Nchi hii iwapo ataacha mifumo iwe inafanya kazi.

=======
Tatizo la Nchi hii sio January, Mwigulu ama Biteko

Kama CCM itaendelea kuongoza Nchi hii hata aje Mtume M.S.W ama Yesu Kristo wa Nazareth kuongoza kupitia Chama hicho basi nao hawatatufaa
Kwani kwenye Uwaziri kuna kubeba Zege!!?Tatizo nchi hii ni vigumu kupata viongozi wazuri kwa sababu ya kubebana bebana. Wengi wapo kenye nafasi hizo kwa kupitia migongo ya wazazi wao au marefa wao ..... ndiyo maana Chawa wanazidi kuongezeka. Yaani huko UVCCM kila kijana ni Chawa. UVCCM ni kiwanda cha kutengeneza CHAWA badala ya viongozi.....!!
 
Raia huwa hawapendi watu wanaofaidi serikali kwa mgongo wa wazazi wao/nepotism
 
Hiyo wizara alianza kwa propaganda na porojo kibao mradi ionekane watangulizi wake hawakufaa anzia bwawani hadi TANESCO.

Kwa sasa mikoani kuna mgao wa umeme wa saa 12 daily tangu 26 August wamejificha kwenye kichaka cha ukarabati kituo cha Ifakara.

Hii issue wala siyo personal.
 
January Makamba, mtoto wa Katibu Mkuu mstaafu wa CCM amekuwa akiandamwa katika mitandao mingi ya kijamii na kujaribu kuaminisha umma ya kuwa ni mtu hafai katika uongozi.

Binafsi Makamba nilimuona wakati wa utawala wa Kikwete akiwa ni mmoja wapo wa wasaidizi wa Rais Kikwete.

Mwenye ushahidi wa wazi kuhusu mabaya yake atuwekee hapa ingawa mimi namuona ni mtu humble, focused na mwenye uvumilivu.
Ni tuhuma tu, hawana ushahidi
 
Watu kila siku wako gizani unategemea waseme nini? Aliingia Wizarani kwa kudanganya umma kuwa wenzake hawakufanya msintenance kwa miaka mitano. Ni kiongozi mmoja wa hovyo sana.
 
Umetumia vigezo gani kusema anafaa? rushwa ni jambo ambalo linafanyika kwa kificho
 
Makamba ni moja viongozi wabovu akifuatiwa na mwigulu angekuwa nje ya mfumo tungekuwa tushamsahau mda mrefu ni mfumo tu wakifamilia unaomlinda

Tanesco hiyo imemshinda pamoja na kupewa pesa nyingi za maboresho na mama lakini migao imeendelea

Mpaka hapa haujiulizi mtangulizi wake aliwezaje hyo wizara
Udini na ufisadi vinamsaidia sn
 
CCM na propaganda duh!! Sasa mbona CAG hakuna huu ufisadi in fact na Tanesco ime record profit kwa mara ya kwanza?

January anaweza akafeli sababu ya incompetence ila kusema ufisadi as if hizo wizara zinazonuka ufisadi kama Madini kule mbona hamkusema Biteko ni fisadi?

Makundi CCM yatawamaliza!!
Tanesco haijapata faida kwa mara ya kwanza..fuatilia taarufa za tanesco hata kabla ya Makamba kuingia.

Kuhusu hicho unachosema hakipo kwenye ripoti ya CAG kwani umeambiwa na pesa ya kwenye vitabu hiyo..hiyo ni rushwa..pale kuna sub contractors companies ambao jamaa kila akitua na private jet lazima wapeleke bahasha.
 
Watu kila siku wako gizani unategemea waseme nini? Aliingia Wizarani kwa kudanganya umma kuwa wenzake hawakufanya msintenance kwa miaka mitano. Ni kiongozi mmoja wa hovyo sana.
Kwanza ni aibu kuwa na kiongozi aina ya Makamba anabebwa na udini pekee
 
Kwani kwenye Uwaziri kuna kubeba Zege!!?Tatizo nchi hii ni vigumu kupata viongozi wazuri kwa sababu ya kubebana bebana. Wengi wapo kenye nafasi hizo kwa kupitia migongo ya wazazi wao au marefa wao ..... ndiyo maana Chawa wanazidi kuongezeka. Yaani huko UVCCM kila kijana ni Chawa. UVCCM ni kiwanda cha kutengeneza CHAWA badala ya viongozi.....!!
Tatizo la Uchawa limezalishwa kutokana na ukosefu wa Ajira miongoni mwa Vijana, ni tatizo lililotengenezwa na Serikali kwa makusudi.

Tatizo hili limepelekea Vijana kushabikia hata mambo ambayo yanaweza kuwa na athari hasi kwao siku za mbeleni bila wao kujua, mathalani ishu ya bandari.
 
Tanesco haijapata faida kwa mara ya kwanza..fuatilia taarufa za tanesco hata kabla ya Makamba kuingia.

Kuhusu hicho unachosema hakipo kwenye ripoti ya CAG kwani umeambiwa na pesa ya kwenye vitabu hiyo..hiyo ni rushwa..pale kuna sub contractors companies ambao jamaa kila akitua na private jet lazima wapeleke bahasha.
Jamaa hawezi kazi hata kidogo
 
Tatizo la Uchawa limezalishwa kutokana na ukosefu wa Ajira miongoni mwa Vijana, ni tatizo lililotengenezwa na Serikali kwa makusudi.

Tatizo hili limepelekea Vijana kushabikia hata mambo ambayo yanaweza kuwa na athari hasi kwao siku za mbeleni bila wao kujua, mathalani ishu ya bandari.
Wao wanawaza kula tu basi kwa siku moja
 
nenda jimboni kwake bumbuli ndio utaelewa Kuwa huyu jamaa hafai hatakuwa mjumbe wanyumba kumi.

Miaka karibu ishirini hajajenga hata hatuamoja yalami ambavyo akienda kuwaomba ubunge anawaahidi kuwajengea lamí🤣🤣🤣
Anajua kule ni wajinga na waoga
 
CCM na propaganda duh!! Sasa mbona CAG hakuna huu ufisadi in fact na Tanesco ime record profit kwa mara ya kwanza?

January anaweza akafeli sababu ya incompetence ila kusema ufisadi as if hizo wizara zinazonuka ufisadi kama Madini kule mbona hamkusema Biteko ni fisadi?

Makundi CCM yatawamaliza!!
Matatizo ya umeme na petrol huyaoni?
 
January Makamba, mtoto wa Katibu Mkuu mstaafu wa CCM amekuwa akiandamwa katika mitandao mingi ya kijamii na kujaribu kuaminisha umma ya kuwa ni mtu hafai katika uongozi.

Binafsi Makamba nilimuona wakati wa utawala wa Kikwete akiwa ni mmoja wapo wa wasaidizi wa Rais Kikwete.

Mwenye ushahidi wa wazi kuhusu mabaya yake atuwekee hapa ingawa mimi namuona ni mtu humble, focused na mwenye uvumilivu.
Haijajulikana chuki yake Ni nin haswa au kauli ile ya baba ake ya wazuri hawafi ndio chanzo Cha chuki
 
Back
Top Bottom