Aisee hali ni tete ndani ya kile chama kilichotamba kwa miaka mingi kuwa ni chama chenye umoja, mshikamano, chenye kuheshimu utu na watu.
Sasa ni mambo ya kuviziana tu. Imefika mahali mwwnachama huyu anataka mwanachama mwenzake afe.
Hii si jambo la kuhendekeza hata kidogo. Chuki na uhasama vimepamba moto.
Ni ccm vs ccm. Wanachogombania ni kile kile
a/ Mgawanyo wa madaraka usio linganifu, hawa wanadae wale wanapewa sana kuliko sisi.
b/ Upendeleo ktk kutoa fursa sawa za kiuchumi. Kundi moja linadhani linafaidi uchumi wa nchi kuliko lingine.
c/ Ndani ya chama upendeleo umezidi kiasi mmoja anaona anamdhulmu mwingine. Inafika hatua sasa hata wajumbe wenye mashina yao wanaowafahamu wagombea wao vizuri hawapewi nafasi ya kupendekeza mgombea sahihi badala yake mgombea anachaguliwa kutoka juu( hili tulionya sasa matunda yake yamekomaa). Mtalinywa.
Matukio yaliyotokea hivi karibuni yameibua hisia za ajabu sana. Kwetu sisi watazamaji tunaona jambo hili sio sawa.
Wote ni wa chama kimoja lakini wanasagiana kunguni kama hawajuani. Kila mmoja anamuona mwenzake ni shetani.
Matukio ya Kufariki Hayati Dr Magufuli, Kufungwa Sabaya, Kushtakiwa Musiba na Kifo cha Membe nadhani Deep statw mnaona kinachoendelea na mnajua solution ni nini. Msijifanye hamuoni. Taifa litatumbukia.
Sasa imefika kuna kundi linaona halina cha kupoteza lolote na liwe ilimradi litaumiza mahasimu bila kujali taifa litaathirika.
Mh Rais kama maridhiano basi yaanze ndani ya chama chako hali ni mbaya. Kuanzia viongozi wa juu hadi wanachama wakawaida.
Nimepitia social media naona wanavyosagiana kunguni najiuliza hawa woote si wachama kimoja?
Kama wanafanyiana hivi je itakuwaje kwa mtu mwenye itikadi tofauti nao?
Je shida ni maslahi? Ni Umaskini? Ni maisha magumu au ni ujinga??
Au kuna mtu anapandikiza haya?