Sikieni binamu mama mkwe ni sawa na mama ako mzazi
Kwanza mheshimu maana bila yy usingepata Mme au mpenzi
Pili Mnyenyekee sana mama mkwe hapa tunaongela sie waafrica mkwe ndo kila kitu we muache hata akikutia kidole cha macho mpotezee tu jenga picha unaweza kumjibu,kumdharau au kmtusi mama yako mzazi?
Tatu usibishane na mama mkwe hata Siku moja haswa kwa mtoto ambae amelelewa na mama tu!maana amepitia tabu zote peke yake!
Cha msingi we piga kimya tu,akutusi akuseme akudharau wee nyamaza!
Mwisho kabisa ukienda ukweni acha Drama jifanye malaika,uvivu weka pembeni!
Fanya kazi km huna akili nzuri!
Ishi nao vizuri,punguza majivuno kua mpole tu!
Ili hata km wakiskia una vituko wasiamini!