Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Warioba sio MTU wa Pwani Wala Dar ,Wala morogoro wala Zanzibar, Wala Lindi Wala mtwara ,kwamba utamkuta ni Mswahili kama ulivyo wewe Kinembe.Za ndaani kabisa ni kwamba Mzee Joseph Sinde Warioba chuki yake ilianza kuumuka baada ya mtoto wake kuondolewa kwenye nafasi ya ukuu wa Wilaya.
Kila akipata fursa lazima afurumushe makombora mazito, lakini chanzo ni hicho.
Mimi naitwa Chiembe, rekebisha jinaWarioba sio MTU wa Pwani Wala Dar ,Wala morogoro wala Zanzibar, Wala Lindi Wala mtwara ,kwamba utamkuta ni Mswahili kama ulivyo wewe Kinembe.
Warioba Ni jabali la Kanda ya ziwa, yuko hivo Toka Enzi na Enzi
Ebu tupia mfano mmoja wa Warioba alivyomfundisha Mwalimu Sheria tufurahi humu.J. S. Warioba alikuwa anabishana na Nyerere wakati Nyerere ni rais na Warioba ni Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Alikuwa anamfundisha sheria Nyerere bila woga, mpaka Nyerere anakubali kushindwa.
Hajaanza hivi karibuni kukosoa uongozi.
Acha siasa za majitaka.
Unahisi ana chuki na serikali, ulitaka afumbe mdomo hata kwa mambo ya msingi ndio uone anaipenda serikali?Za ndaani kabisa ni kwamba Mzee Joseph Sinde Warioba chuki yake ilianza kuumuka baada ya mtoto wake kuondolewa kwenye nafasi ya ukuu wa Wilaya.
Kila akipata fursa lazima afurumushe makombora mazito, lakini chanzo ni hicho.
Kwani kazi ya kumjibu Mzee bado ni zamu yako?Kwenu hamna Wazee?Za ndaani kabisa ni kwamba Mzee Joseph Sinde Warioba chuki yake ilianza kuumuka baada ya mtoto wake kuondolewa kwenye nafasi ya ukuu wa Wilaya.
Kila akipata fursa lazima afurumushe makombora mazito, lakini chanzo ni hicho.
Wakati Warioba ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Nyerere alikuwa anataka kumfunga mtu fulani kwa sababu zake.Ebu tupia mfano mmoja wa Warioba alivyomfundisha Mwalimu Sheria tufurahi humu.
Maana mimi ninachojua kwa Mzee Warioba ni kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa ubunge mwaka 1990 Jimbo la Bunda kabla ya mahakama kutengua ubunge wake! Ahahahahaha!!!
Watoto wa 2000 mna shida sana, hivi Warioba umemjua juzi? Hebu uliza alivyokuwa ananyoosha system since way back, alikuwa PM era ya Mwinyi lakini alikosoa kila alichokiona hakiendi vizuri ilhali alikuwa kwenye system.Za ndaani kabisa ni kwamba Mzee Joseph Sinde Warioba chuki yake ilianza kuumuka baada ya mtoto wake kuondolewa kwenye nafasi ya ukuu wa Wilaya.
Kila akipata fursa lazima afurumushe makombora mazito, lakini chanzo ni hicho.
Kama mambo yanaenda shagalabagala anyamaze?Awamu hii kazidi,awamu ya tatu,nne,tano hakuwa hivi
Pius Msekwa je?Butiku anajihami, hataki auditing ya Mwalimu Nyerere Foundation ambayo kajifanya Mwenyekiti wa kudumu. Skolashipu zote za china na urusi anawapa wazanaki na ndugu zake
Vijana wa juzi hamumjui Warioba, enzi hizo mpaka kila mja aliamini anakula ndumu kwa jinsi alivyokuwa hamung'unyi maneno. Siku hizi amekuwa soft kidogo nadhani ni sababu ya umri.Awamu hii kazidi,awamu ya tatu,nne,tano hakuwa hivi
The so called Gen Z hawawezi kukuelewa, wanakurupuka pasina kujua lolote.Wakati Warioba ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Nyerere alikuwa anataka kumfunga mtu fulani kwa sababu zake.
Yule mtu akafunguliwa mashitaka mahakamani, akashinda, Nyerere akaamuru ashikwe upya asomewe shitaka lile tena. Warioba akamkatalia Nyerere, akamwambia hatuwezi kufanya hivyo mzee, huyu mtu kashashitakiwa kapatikana hana hatia, kumshitaki tena ni "double jeopardy". Sheria inakataza. Nyerere akalalamikia sheria lakini ikabidi akubali tu.
Kuna stories nyingi tu, kuna siku ya kuzindua kitabu cha Sokoine, Warioba alihadithia jinsi akivyopingana na Sokoine kwenye sheria za wahujumu uchumi zikivyokuwa zinavunja haki za binadamu mpaka wakapelekana kwa Nyerere.
Kwa hivyo, Warioba hajaanza kukosoa wakubwa serikalini leo wala jana, kashafanya hivyo tangu enzi za Nyerere na Sokoine.
Zaidi, jadilini hoja jamani, acheni kumjadili mtoa hoja.
Kumjadili mtoa hoja badala ya hoja ni logical fallacy, ad hominem fallacy.
Ni tabia ya watu wasio na hoja.
Awamu ya kwanza ni ya mjomba wake,awamu tatu,nne,tano nilikua mtu mzima tuVijana wa juzi hamumjui Warioba, enzi hizo mpaka kila mja aliamini anakula ndumu kwa jinsi alivyokuwa hamung'unyi maneno. Siku hizi amekuwa soft kidogo nadhani ni sababu ya umri.
Kuna kipi kinaenda shaghala baghala leo na hakikufanyika awamu ya tano?Kama mambo yanaenda shagalabagala anyamaze?