Chuki za Roy Hodgson kwa wachezaji wa Leicester city kuiondoa England mapema euro 2016

Chuki za Roy Hodgson kwa wachezaji wa Leicester city kuiondoa England mapema euro 2016

Stelling na Wilshere hata benchi wasingekaa! Kikosi mbele lazima kingekuwa na 4-4-2 mbele Vardy na Kane pmbeni Roney na Milner,kati Dier na Ali hapo full mzigo anapigwa yoyote
Naam kwa mbaali England ingeleta Burudani
 
England hata wafundishwe na nani, hawana wanachojivunia zaidi ya history ya mwaka sijui mwaka gani walichukua world Cup karne sijui ya ngapi vile,
Hata sijui ni historia ipi wanayoivunia maana hawajawahi kushinda kombe la Euro tangu lianzishwe mwaka 1960. sasa zimepita fainali 24. England haijawahi kuchukua ubwingwa.

England wamewahi kuchukua kombe la dunia Mara moja, mwaka 1966 ambapo walikuwa wenyeji na waliifunga West Germany 4-2 kwenye uwanja wa Wembley

Labda tuseme Urusi wanajisifia kwa historia ya iliyokuwa Soviet Union maana iliwahi kuchukua kombe la Euro mwaka 1960 wakati likianzishwa nchi ufaransa. Ingawa kulikuwa na timu nne tuu bado imekuwa rekodi ya kujivunia kwa iliyokuwa Soviet Union na kwakuwa Urusi ndio successor wa sehemu kubwa wa iliyokuwa Soviet Union basi imekuwa ikitengemea historia hiyo ingawa si timu bora katika historia ya mpira wa miguu. Na ndio maana hata ile sare ya Jana walishangilia sana kama wamechukua ubingwa vile.
 
nilidhan vardy yuko injured...???? Ila kama kajisikia kufanya hvyo...bhas ajiandae kwenda kufundisha derby country
 
England hata wafundishwe na nani, hawana wanachojivunia zaidi ya history ya mwaka sijui mwaka gani walichukua world Cup karne sijui ya ngapi vile,

Ilikuwa mwaka 1966 na England walinyakua kombe hilo ambapo waliwafunga Germany 4-2 katika dakika za nyongeza.

Mechi ilikuwa uwanjani kwao Wembley na mfungaji wa goli la tatu aliotea lakini goli hilo likapitishwa na mwamuzi na mshika kibendera wake ambao walikuwa ni warusi.

Mpaka dakika 90 zinakwisha goli zilikuwa ni 2-2 na zikiwa dakika 11 zimekwenda ndani ya muda wa nyongeza, mshambuliaji wa Engalnd Geoff Hurst akapiga shuti likagonga besela na kurudi uwanjani ambapo beki wa Germany akaukoa.

Lakini mwamuzi na mshika kibendera wake wakaamua kuwa hilo ni goli, na sheria ya mpira inasema kwamba mpira mzima ni lazima uingie wavuni ili ihesabiwe kuwa ni goli.

Baada ya goli lile Germany walikata tamaa sana na wakaruhusu goli linguine la nne na kushindwa mechi hiyo.

Lakini wakti ule kulikuwa na siasa nyingi sana na ndio maana lile goli lao la tatu "limewaathiri sana"(labda Germany walinuizia) mpaka leo England hawajapata bahati ya kushinda kombe la dunia.

Na hili jambo linawasumbua sana England mpaka kesho na bado wana uhasama wa chinichini juu ya tukio lile.

Muingereza akikusikia unatajataja Germany kwa suala la mpira kwa kuwasifia anaweza asiwe rafiki yako kihivyo..
 
Kwani aliyeteua wachezaji wa kuunda Three Lions ni nani kama sio Hodgson mwenyewe?
Iweje ndani ya mechi moja hii ambayo mdai kuwa anawachukia wachezaji wa Leicester City? Quite unfair.

Vv
 
Sasa ni dhahiri kwamba kocha huyu kikongwe anazo chuki binafsi.

Katika hali ya kawaida huwezi kumwacha benchi Jamie Vardy kama unataka kushinda , hii ni ajabu !

Ukiangalia kwa makini Vardy kila nafasi anayopata ndani ya 18 hesabu ni goli , habahatishi , kwenye game kama hizi usitarajie kupata nafasi nyingi sana , kwahiyo unahitaji mchezaji mwenye uwezo na asiyefanya ajizi kama Vardy .

First touch yake haina mfano , sasa unamuachaje benchi ?

Alimuacha DrinkWater akaleta mshangao dunia nzima , sasa hii shilingi nyingine anayoichezea itamrudisha nyumbani mapema sana , Hakuna striker wa England wa kumuweka benchi Vardy , utake usitake .

Roy Hodgson amewapendelea Harry Kane na Wayne Rooney na hawa hawakuwa makini zaidi kwenye umaliziaji.

England jana wameonyesha kwamba walikosa kiongozi uwanjani na hili pia ni tatizo.

Nafikiri atabadilisha timu dhidi ya Wales lakini hawezi kumuacha Rooney kwenye bench.

Ila madai yako kwamba Hodgson ana chuki juu ya Vardy naona kwamba "it's a bit harsh".
 
Vardy aanze na kane Mbele timu haibalance hapo halafu kuna mamluki wengi wanajifanya wanaipenda England em tuachieni timu yetu
 
England wangekuwa na timu kama Belgium tu basi nadhani timu zote zingekoma pale ufaransa
 
England hata wafundishwe na nani, hawana wanachojivunia zaidi ya history ya mwaka sijui mwaka gani walichukua world Cup karne sijui ya ngapi vile,

England ni kama wa Matopeni tuu,wanajivunia historia ya nyuma na kucheza mpira mdomoni.
 
Kwani aliyeteua wachezaji wa kuunda Three Lions ni nani kama sio Hodgson mwenyewe?
Iweje ndani ya mechi moja hii ambayo mdai kuwa anawachukia wachezaji wa Leicester City? Quite unfair.

Vv
Kama anapita hapa jf ajionee jinsi alivyoboronga
 
Tumpe nafasi ukiangalia ata beki yao chini ya smalling ni mbovu.
 
Stelling na Wilshere hata benchi wasingekaa! Kikosi mbele lazima kingekuwa na 4-4-2 mbele Vardy na Kane pmbeni Roney na Milner,kati Dier na Ali hapo full mzigo anapigwa yoyote
Naona hiyo timu haumii mtu na haina sub!tuseme tu England timu Yao ni yakawaida tu imekosa wachezaji wakuwapa matokeo..
 
Mie nilishangaa sana Vardy kutoanza jana hasa ukitilia maanani performance yake kwenye BPL. Wasipobadili upangaji wa timu basi wanaweza kabisa kufungishwa virago vyao mapema sana. Na majanga ya timu yao ya Taifa kuendelea.
 
Ilikuwa mwaka 1966 na England walinyakua kombe hilo ambapo waliwafunga Germany 4-2 katika dakika za nyongeza.

Mechi ilikuwa uwanjani kwao Wembley na mfungaji wa goli la tatu aliotea lakini goli hilo likapitishwa na mwamuzi na mshika kibendera wake ambao walikuwa ni warusi.

Mpaka dakika 90 zinakwisha goli zilikuwa ni 2-2 na zikiwa dakika 11 zimekwenda ndani ya muda wa nyongeza, mshambuliaji wa Engalnd Geoff Hurst akapiga shuti likagonga besela na kurudi uwanjani ambapo beki wa Germany akaukoa.

Lakini mwamuzi na mshika kibendera wake wakaamua kuwa hilo ni goli, na sheria ya mpira inasema kwamba mpira mzima ni lazima uingie wavuni ili ihesabiwe kuwa ni goli.

Baada ya goli lile Germany walikata tamaa sana na wakaruhusu goli linguine la nne na kushindwa mechi hiyo.

Lakini wakti ule kulikuwa na siasa nyingi sana na ndio maana lile goli lao la tatu "limewaathiri sana"(labda Germany walinuizia) mpaka leo England hawajapata bahati ya kushinda kombe la dunia.

Na hili jambo linawasumbua sana England mpaka kesho na bado wana uhasama wa chinichini juu ya tukio lile.

Muingereza akikusikia unatajataja Germany kwa suala la mpira kwa kuwasifia anaweza asiwe rafiki yako kihivyo..
England hakuna mpira ila kuna promo tuu ndio maana ligi yao ni maarufu duniani ila haina ubora wowote kulinganisha na Laliga, Bundesiliga nk... Promo nyingi kutoka kwa media za kiingereza ndo zinafanya ligi yao iwe na umaarufu.

Wingereza hakuna wachezaji wenye uwezo na vipaji vya hali ya juu kulinganisha na mataifa kama Ujerumani, Ufaransa, Uhispania, Ureno, Uholanzi nk..... Wamezoea kubebwa na kujisifu tuu kupitia media zao .
 
Wewe ungekuwa ndiyo kocha wa Uingereza, ungechezesha wachezaji gani? Tupia kikosi chako cha kwanza na akiba!
ndio maana kina Gary Neville, Jamie Carragher,akina Henry wapo,kwa performance ya vardy Sio ya kumuweka bench 90' min
 
Nadhani kama angekuwa hamuhitaji (kwa chuki kama ulivyoandika) basi asingemwita kabisa kikosini.

Nadhani kocha mwenyewe anajua kwanini hakumchezesha.
angewezaje kumuacha among Three Top scorer wa EPL msimu ulioisha na bingwa pia mchezaji bora wa ligi aliogopa hisia za Waingereza,..na kumuita kwake sio kwamba hana chuki nae ( kama ipo)
 
Back
Top Bottom