Chukua muda wa kuzipumzisha hisia

Chukua muda wa kuzipumzisha hisia

Dah pole sana, yaani mpaka alwatan kama wewe unalizwa kwenye mapenzi.....basi nanyanyua mikono juu ya penzi. Nausikia ule wimbo usioisha utamu wa Muumin ukiimba akili mwangu...."Nilipokuwa mtoto, nilifikiri penzi ni Jabari ambalo linaweza ua....Tunda Special." Muumin ni kiboko na aliutendea haki huu wimbo.
Naomba nitafutie huu wimbo NAFSI YA KUDHANI... by Hafsa kazinja
 
OTE="UngaUnga, post: 25342552, member: 266495"]Yaani ww Expert Member wa jf hata kummention Joowzey kuwa unamuita unashindwa![/QUOTE]
Cha ajabu hasa hapo ni kipi!??
 
Bro hujuagi kuongea pumba.uzi umelenga moja kwa moja hisia na maisha yng halisi.kula 5 [emoji109][emoji109][emoji109]
 
Usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya baada ya kuumizwa na mtu uliyempenda sana uliyemwamini sana, uliyemsaidia sana na uliyemvumilia sana na bila huruma akaamua kuondoka ama kukuumiza wakati ulipokuwa unamhitaji sana

Mapenzi yanaumiza mapenzi yanatesa lakini ni muhimu kuangalia ulikotoka.. Maisha yako ni muhimu kuliko yeye.. Hakuwapo Kabla... Kisha akaja... Mwache aende... Future yako yaweza kuwa muhimu kuliko yeye...

Umewekeza kwake sawa... Ulimkabidhi moyo wako sawa.. Lakini kama hana hisia nawe, kama hana shukrani... Kama hakupendi tena na kama kakutenda mwambie waweza kwenda... Akuachie japo pumzi yako... Isifike mahali nayo akaondoka nayo...!!!

Ili kutambua upande wa pili wa mapenzi ni lazima kuumia ni lazima kuumizwa.. Usione ndio mwisho wa maisha, chukulia kama ni changamoto... Mitihani ya dunia

Wewe si wa kwanza hutakuwa wa mwisho... Vumilia... Muda pekee ndio utayaponya majeraha ya mapenzi... Usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya unaweza kuingia chaka... Utafanya hivyo kwa ghadhabu na bila fikra timilifu.. Unaweza kuongeza tatizo badala ya kuponya majeraha....

Zipumzishe hisia... Mapenzi yanachosha sana... Jipe muda wa kutafakari upya... Ulipokosea ulipopatia, uliposhindwa kutimiza wajibu... Ulipotenda kwa weledi na chochote utakachoweza kutafakari... Baada ya kuona umepata nguvu ya kuanza tena... Fanya hivyo bila papara... Epuka uzuri wa mkakasi.....

Zijapopita siku za furaha usihuzunike bali ufurahi kwakuwa zilikuwako.. [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji779] [emoji781] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770]
Kaka naona maumivu yamezidi,lakini hayakimbiwi ila pambana nnayo hatimaye utashinda(utasahau tu).Unaondokewa na kipenzi chako wa roho MZAZI aliyekuzaa na aliyekukukuza lakini inafika mahali akili inakubali kuwa hili limetokea na limeisha,sembuse mmekutana ukubwani unalalama eti huwezi kusahau,.Acha kuendekeza moyo,kubali matokeo utaona nafsi inarizia yalitokea.Mshana upo brother
 
Kaka naona maumivu yamezidi,lakini hayakimbiwi ila pambana nnayo hatimaye utashinda(utasahau tu).Unaondokewa na kipenzi chako wa roho MZAZI aliyekuzaa na aliyekukukuza lakini inafika mahali akili inakubali kuwa hili limetokea na limeisha,sembuse mmekutana ukubwani unalalama eti huwezi kusahau,.Acha kuendekeza moyo,kubali matokeo utaona nafsi inarizia yalitokea.Mshana upo brother
Asante kwa ushauri na kunitia sana moyo.. Hii ni mada tu maalum kwa wale wanaopitia nyakati ngumu na kutendwa ama kusalitiwa katika mahusiano... Ni kwa ajili ya wale wote wanaohitaji faraja na ushauri....the moment of truth, mwambie waweza kwenda
 
naona kila anaepita humu anasema ujumbe umekuja wakati muafaka...aisee kweli mapenzi hayana mwenyewe![emoji1]

poleni mnaopitia ktk huo wakati ndio maisha yenyewe hayo, kaka mshana jr asante kwa kutukumbusha.

ila tuache ubishi....kama akienda muache tu usilazimishe mapenzi.
 
Broo sitaki ugomvi na wewe huu Uzi umeanzisha kwa ajili yangu wee poa tu
 
Back
Top Bottom