Darmian
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 17,289
- 46,624
Maybe inawezekana..Nimetoa milioni 4.5 kwa wakala nmb, master card
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maybe inawezekana..Nimetoa milioni 4.5 kwa wakala nmb, master card
Nilitarajia kuona mtuhumiwa kachakaa kwa kipondo. Atawezaje kufunguka bila kiposongo kwa mfano?
Hongera kwa wakala aliesaidia kukamatwa kwa jizi hili.
Not may be.... tunavyoongea tu nimetoka kutoa 1.5M kwa wakalaMaybe inawezekana..
Unasomaga details za ATM card yako kabla na baada ya kuitumia? ShitukaHata sijaelewa asee
Asee Mika ni Uncle wangu, Kama si mkewe angekufa kwa kihoro, ila amepata taabu sana asee, maana yake kama alidata flank hivi.Taarifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa wizi kwenye mashine za kutolea fedha benki (atm) mnamo tarehe 25/10/2019 katika kituo cha polisi Mbagala maturubai, mzee Ernest Mika Sakala, ambaye ni afisa mwandamizi mstaafu wa jeshi la polisi alitoa ripoti kwamba tarehe 23/10/2011 majira ya 10:00hrs alibadilishiwa kadi yake ya benki ya crdb na kupewa ya mtu mwingine bila yeye mwenyewe kufahamu, wakati alipokwenda kutoa fedha kwa wakala wa benki hiyo ambaye anaendesha biashara yake maeneo ya Dar live Mbagala Zakh-em.
Kwamba siku mbili baadae aligundua kuwa kadi ya benki aliyo nayo siyo yake, na alipokwenda kufuatilia benki ya crdb Mbagala siku ya tarehe 25/10/2019 aligundua kuibiwa kwa fedha kutoka kwenye account yake kiasi cha tzs. 10,000,000/=. Fedha hizo zilitolewa kwa mawakala watatu tofauti siku ya tarehe 23 na 24 october, 2019. Upelelezi wa shauri hili ulianza kufanyika, ambapo mawakala ambao fedha zilitolewa na baadhi ya maafisa wa benki walihojiwa. Pia CCTV footages zilizomuonyesha mtuhumiwa wa kike aliyeonekana kutoa fedha kwa kutumia kadi hiyo iliyoibiwa kutoka kwa wakala mmoja wapo.
Wakati upelelezi ukiendelea, tarehe 19/11/2019 katika benki ya crdb Mbagala wakala mmoja akiwa katika maeneo ya benki hiyo alimtilia shaka dada mmoja aliyeonekana kwenye atm za benki hiyo akijaribu kutoa fedha, na alipomsogelea na kuanza kumuhoji dada huyo alijaribu kukimbia, lakini aliweza kudhibitiwa. Polisi walipewa taarifa na bila kuchelewa polisi walifika eneo hilo la benki na kumkamata dada huyo.
Alipofikishwa kituoni na kupekuliwa, alikutwa na jumla ya kadi 23 za watu na benki tofauti akiwa ameziweka kwenye kipochi kidogo na kuzisokomeza ndani ya uke wake. Mojawapo ya kadi alizokutwa nazo ni ya mzee Ernest Mika Sakala. Kadi hizo zipo katika mchanganuo ufuato:
1. CrdB- kadi 07
2. Nmb- kadi 06
3. Nbc- kadi 02
4. Amana- kadi 02
5. Posta- kadi 02
6. Acb- kadi 01
7. Stanbic- kadi 01
8. Dtb- kadi 01
9. Equity- kadi 01
Katika mahojiano, mtuhumiwa huyo ameeleza kwamba yeye na watuhumiwa wenzake, ambao bado tunawafuatilia, wamekuwa waki-target watu wenye umri mkubwa (wazee) na wastaafu ambao huenda kwenye mashine za atm na kushindwa kuzitumia hivyo kuomba msaada kwa mtu wa pembeni. Kwamba wakati wanapowasaidia kutoa fedha, kwa kutumia ujanja wanakariri namba za siri, na baada ya kufanya muamala wanachukua kadi ya muhusika na kuificha, na kumueleza kuwa kadi imemezwa kwenye mashine. Hivyo basi, victim anapoingia ndani ya benki kufuatilia kadi yake, wao wanaondoka na kadi kwenda kwa wakala yoyote yule au kwenye mashine nyingine ya atm kuangalia salio na kuanza kutoa fedha.
Mbinu nyingine ni kuwafuatilia wateja wanaokwenda kutoa fedha kwa mawakala, na kukaa pembeni yao na kuchungulia pindi mteja anapoingiza namba yake ya siri. Baada ya hapo mteja akishapewa fedha na wakala anakuwa busy kuweka mfukoni fedha alizopewa, huku kadi yake akiwa ameicha mezani, na hapo ndipo wanatumia mbinu ya kumbadilishia na kumuwekea kadi ya mtu mwingine ambayo tayari fedha zake wanakuwa walishaziiba. Amekana kushirikisha afisa yeyote wa benki au wakala katika kufanikisha wizi huo. Upelelezi bado unaendelea.
View attachment 1268455View attachment 1268457
10m zinatokaje kwa wakala ndani ya siku tatu??..au hiyo card ilikuwa Platnum??..maana kadi za kawaida kutoa haizidi 1.2m per day,,
Nenda wakala wa CRDB unatoa hata 3mHii ngumu kumeza
Labda walienda na bank kuwith draw
In 3 days up 18m unaweza toa asee. Acha kabisa.10m zinatokaje kwa wakala ndani ya siku tatu??..au hiyo card ilikuwa Platnum??..maana kadi za kawaida kutoa haizidi 1.2m per day,,
kwa wakala unatoa hta 20m sema makato ndo makubwaHii ngumu kumeza
Labda walienda na bank kuwith draw
Mkuu Kama K inaweza kutoa Toto la 5kg ATM card kitu ganiSijaelewa hapo kwenye kuweka kadi ukeni...imewezekana vipi ??
Duka lake lipo maeneo gani mkuu?maweee
huyu sista kumbe ni panja!?
halafu ukimuona u can't believe!
ana shop lake la nguo zile pamba kaliii; na usafiri wake ni harrier nyeusi tii.
aaaiiissseeeee
Kuna wakala yupo vizuri hapo kkoo hata ukitaka mil 50 anakupa,sijamuelewa mleta UziNimetoa milioni 4.5 kwa wakala nmb, master card