Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti?

Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti?

Hahaha kuna shosti aliweka mdada kwenye mpesa stall. Da kabwenga mtaji wote wa milioni 3. Anaulizwa anasema ni chuma ulete. Nimecheka tu, manake ningekuwa mie nahisi ningemtia ndani
kwani chumaulete imekuwa proved scientifically ?
 
hizi ni njia ambazo unaweza kuzitumia kuepusha pesa zako zisipotee kimazingara.. Tumia mojawapo pale unapomshitukia/unawasiwasi nae...
1. Pindi unapopewa pesa jitahidi usiichanganye na pesa nyingine, kwa mda fulani.
2. Unapompa change usimpatie mkononi, iweke mezani ajichukulie/aichukue mwenyewe. Hii njia hutumika sana na wafanyabiashara madukani
3. Ile pesa ichane kwenye angle, chana kipande kidogo sana, kama vile unatoa angle, tumia ukucha kuitoa angle ,

Dawa ni kuziombea pesa zako na kuzitakasa..Hakuna nguvu iishindayo ile ya Bwana Mungu wetu. Na si kwa hizo peke yake ombea hata pesa uwapazo omba omba mengine ni mapepo tu
 
Oooh kumbe ndo maana ukilipa au kurudishiwa change mtu anatupia juu ya meza? Huwa nakereka sana hii tabia, sikua najua wanamaanisha nini..loh

ukiona hivyo jua jamii ina mashaka na wewe.......isije ikawa una mbinu hizo..?ha ha ha...
 
Daah...sasa ndio nimefumbuka. niliwahi kununua nguo kwenye duka moja, niling'ang'anizwaje kuweka hela juu ya counter?! Kumbe nilionwa chuma ulete! Aisee...
 
Kwenye biashara hii kitu ipo,
unaweza kupewa noti ya elfu kumi ukiiichanganya tu na pesa nyingine umekwisha,
au mtu anakuomba chenji ukiichanganya ile pesa na pesa zako ujue umeliwa
 
hizi ni njia ambazo unaweza kuzitumia kuepusha pesa zako zisipotee kimazingara.. Tumia mojawapo pale unapomshitukia/unawasiwasi nae...
1. Pindi unapopewa pesa jitahidi usiichanganye na pesa nyingine, kwa mda fulani.
2. Unapompa change usimpatie mkononi, iweke mezani ajichukulie/aichukue mwenyewe. Hii njia hutumika sana na wafanyabiashara madukani
3. Ile pesa ichane kwenye angle, chana kipande kidogo sana, kama vile unatoa angle, tumia ukucha kuitoa angle ,

Uswahili Mtupu! Watanzania Tuachane Na Hizi Imani Kikubwa Mwombe Tu Mwenyezi Mungu Na Tujifunze Kujiamini.
 
Wenye Akili Zao Wametutengenezea Pesa Za Noti Sisi Waswahili Kwa Imani Zetu Za Kimasikini Na Kiswahili Eti Tunazikata ktk Kingo! Sasa Tukate Pesa Zote Zilizoko ktk Mzunguko Wake? Binafsi Huwa Nachukia Mtu Anayeendekeza Hizi Imani Na Bahati Mbaya Mno Watanzania Sasa Tumeshaathiriwa Na Ushirikina Na Laiti Kama Mambo Haya Yangekuwa Ya Kweli Basi Kuna Mikoa Hapa Tanzania Ina Hizo Sifa Lakini Cha Kushangaza Ndiyo Mikoa Masikini Na Ina Wakazi Wengi Wasio Na Elimu!
 
C mbona dukan kwetu tumeweka biblia tu na hakuna cha hasara wala nn na faida kila cku inaonekana nzur tu..... na kila mtja ela anapewa mkonon...kila kitu ni iman.c tunamwamin YESU KRISTO
 
Mm alishakuja mtoto mdogo dukani kwangu kununua mafuta ya nywele alikuwa ameandikiwa mafuta anayohitaji ktk karatasi nikampa mafuta na chenji yake na ndio alikuwa mteja wangu wa mwisho siku hile, kesho yake nikakuta hirizi ktk box la pesa halafu pesa zote hazipo. Nikaichoma moto.
 
Wewe unamtumikia Mungu katika Roho na Kweli?

Au unataka Mungu akubariki tu kwenye biashara yako wakati zaka na sadaka hautoi?

Mungu habariki mtu kwa sadaka Tu.Yeye alisema ombeni lolote kwa jina langu aminini mtapata hakuweka sharti lingene lolote ILA aminini ntu
 
Back
Top Bottom