DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Kuna haka katabia kalianza kunikera katika vilabu vya Simba na Yanga ka viongozi wa siasa kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji baada ya mechi na wakati mwingine kabla ya mechi na hata kipindi cha mapumziko.
Ni katabia kalikoota mizizi na sasa imeonekana kama ni jambo la kawaida tu na kamehamia kwenye timu ya taifa.
Vyumba vya kubadilishia nguo ni sehemu special sana kwa wachezaji na benchi la ufundi. Ni sehemu wanapoweza kujiachia wao wenyewe, wakakosoana, wakapeana moyo na kurekebishana. Panapotokea ushindi muhimu ni sehemu yao pekee special ya kusherehekea pamoja wenyewe bila kujali nani yupo around anawachungulia au anawashobokea.
Kwa wenzetu, hata viongozi wa juu wa vilabu huwa huwakuti wakiingia kwenye vyumba vya wachezaji.
Huu utaratibu wa wanasiasa kuingia huko vyumbani ni wa hovyo na ni muendelezo wa tabia ya kutafuta umaarufu mrahisi rahisi tu kupitia michezo. Mna nafasi na sehemu nyingi za kuongea na hao wachezaji, tumieni hizo na waacheni huko vyumbani wakae wenyewe kama utaratibu ulivyo duniani kote.