DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Wanasikilizia. Fursa ikijitokeza hawaachi ipite hivi hivi. Aibu ikitokea wanatelekeza timuTimu Ikiboronga Huwaoni Ng'ooo...Ishinde Sasa Hadi Keroo Na Matumbo Yao...
Tunaendesha mpira wetu katika ngazi kubwa kama hizi kama vile vitimu vya mtaani. Vitimu vya mtaani wakati wa mapumziko, wakikaa pale kwenye nyasi katika mduara, kila mtu anasogea kuongea.....shabiki, muuza madafu, diwani, mwenyekiti wa mtaa, mganga wa timu, demu wa kepteni, muuza maji, kocha kama wanaye, kila mtu anatoa ushauri na unasikilizwa!Ukombozi kifikra ni muhimu sana
Wanatambiana msibani bila haya iwe michezoni.Kuna haka katabia kalianza kunikera katika vilabu vya Simba na Yanga ka viongozi wa siasa kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji baada ya mechi na wakati mwingine kabla ya mechi na hata kipindi cha mapumziko.
Ni katabia kalikoota mizizi na sasa imeonekana kama ni jambo la kawaida tu na kamehamia kwenye timu ya taifa.
Vyumba vya kubadilishia nguo ni sehemu special sana kwa wachezaji na benchi la ufundi. Ni sehemu wanapoweza kujiachia wao wenyewe, wakakosoana, wakapeana moyo na kurekebishana. Panapotokea ushindi muhimu ni sehemu yao pekee special ya kusherehekea pamoja wenyewe bila kujali nani yupo around anawachungulia au anawashobokea.
Kwa wenzetu, hata viongozi wa juu wa vilabu huwa huwakuti wakiingia kwenye vyumba vya wachezaji.
Huu utaratibu wa wanasiasa kuingia huko vyumbani ni wa hovyo na ni muendelezo wa tabia ya kutafuta umaarufu mrahisi rahisi tu kupitia michezo. Mna nafasi na sehemu nyingi za kuongea na hao wachezaji, tumieni hizo na waacheni huko vyumbani wakae wenyewe kama utaratibu ulivyo duniani kote.
Nilisikia lakini mtu akisema huku mtandaoni ni 16% ambapo 40% wanaishi nje na hawana mpango wa kurudi nchini. Ndivyo wanavyolichukulia TaifaTunaendesha mpira wetu katika ngazi kubwa kama hizi kama vile vitimu vya mtaani. Vitimu vya mtaani wakati wa mapumziko, wakikaa pale kwenye nyasi katika mduara, kila mtu anasogea kuongea.....shabiki, muuza madafu, diwani, mwenyekiti wa mtaa, mganga wa timu, demu wa kepteni, muuza maji, kocha kama wanaye, kila mtu anatoa ushauri na unasikilizwa!
Hilo nimelisema kitambo sana. Pia kutoa pesa vile inaonyesha pesa yetu haina thamani au kiwango kinachotolewa ni kidogo sana kwa mtazamo wao au hawawaheshimu wachezaji.Leo umeongea pointi. Hata ule utoaji hadharani wa maburungutu ya hela nao ni wa kishamba.
Kama wachezaji wamewaahidi kiasi fulani cha fedha kama motisha iwapo watashinda, basi kiwekwe moja kwa moja kwenye akaunti zao. Binafsi sioni kama kuna sababu ya msingi ya kujirekodi na kuanza kusifiana wakiwa na hayo maburungutu ya hela, huku wakiwakabidhi wachezaji.