Huyu nilimuona kawa ndugu kwani tumekua mtaa mmoja, shule moja, tuition moja, darasa moja na mkondo mmoja ingawa darasani tulitofautiana madawati. Katika makuzi yetu ilifikia hatua hata mama zetu wakawa wanafahamiana, tukaachana tulipoingia sekondari.
Muda ukapita, bado tukiwa marafiki haswaa, tukishirikiana katika mambo mbali mbali. Madem zangu asilimia kubwa alikuwa anawajua either kwa stori au kwa kuwaona. Nasikitika kusema kuwa ni miaka 9 sasa imepita, ule urafiki, uthamani na undugu uliokuwa kati yetu haupo na wala hautakuja kuwepo kwa maisha yangu yaliyobaki duniani.
Kuna demu nilimpata nikawa nadate nae, ikafikia hatua nikamtambulisha kwa jamaa sababu alitaka kumsalimia siku moja sababu nilimwambia siku moja jamaa ni mgonjwa, wakasalimiana na mengine yakaendelea. Yule bibie penzi lilikufa, jamaa urafiki ukafa, sijuagi mpaka leo kama wanaendelea au waliachana ila huwa namuomba Mola tu awabariki.
2013 nilipitia kipindi kigumu na kizito sana. Hakuna siku nitakuja kusahau kipindi hiko.