Je, unapenda kukamua chunusi zilizokuandama usoni ili ziishe? Kama jibu ni ndio, basi acha kufanya hivyo mara moja! Tabia ya kukamua chunusi usoni mara kwa mara yanaweza kukuletea
madhara ya ngozi. Utapata vitundu kwenye ngozi yako ya uso vya kudumu na havitotoka tena kama utaendelea kukamua chunusi (huitwa permanent scarring of your face). Hata uende kwa
wataalam wa ngozi wanaweza kushindwa kuondoa hizo alama zilizosababishwa na kukamua chunusi. Kukamua chunusi pia kunasababisha ngozi yako kuondokewa na kinga ya kuzuia bacteria ambayo itakusababishia maambukizi mapya na ngozi (severe infections).
Kama inakubidi chunusi zako kuzikamua, basi nenda kwa mtaalam (facial expert) wakaziondoe kwa kutumia vichuma maalum (pimple extractor), anti-bacteria solutions (gel za kuzuia backteria) na lotion au cream ya kutibu chunusi (Acne treatment ointment or cream).
Kama muda au uwezo wa kwenda salon huna, basi tumia maujanja yafuatayo;
1. Acha kukamua chunusi zako hovyo, ukiwa kazini, kwenye daladala, ukiwa ukitazama TV, ukiwa kitandani, na kadhalika. Achana na tabia hiyo maana utajiharibu sura yako!
2. Acha tabia ya kujigusa gusa uso wako kila wakati, hasa kama unazo chunusi tayari
3. Watu wengi wanaopata chunusi wana ngozi za mafuta (Oily skin) hivyo watu hawa wanapaswa kuachana kabisa na vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi. Mfano chipsi, vyakula vya kukaangwa na mapipi, biskuti, nakadhalika. Uamuzi ni wako, chagua kunyoa au kusuka. Utamu wa kuridhisha tumbo/kinywa chako au uso soft.
4. Tumia mafuta au lotion usoni iliyoandikwa 'Oil Free' au 'For Oily Skin'. Ukitumia mafuta yaliyoandikwa 'For Dry Skin' unakuwa unjaiongezea mafuta zaidi kwenye uso wako, hivyo kusababisha uzalishaji wa sebum, ambayo ni chembechembe inayozalisha chunusi.
5. Tengeneza mask mara moja kwa wiki ujifanyie tiba mwenyewe ya asili ukiwa nyumbani. Nunua fungu la majani mabichi ya giligilani (huuzwa sokoni), chambua nusu yake, kisha pima vijiko viwili
vya kulia chakula vya unga wa Manjano. Pondaponda majani ya giligilani (fresh coriander leaves) uchanganye na unga wa manjano (turmeric powder), kamulia na kipande cha ndimu, kisha upake
kwenye chunusi zako na ukae nayo usoni kwa muda wa dakika 10. Kisha nawa uso wako kwa maji ya vuguvugu na upake 'Oil free cream' au lotion yako ya kutibu chunusi. Acne cream and Acne
lotion. Fanya hivi kila wiki kwa muda wa mwezi mzima na utaona alama nyeusi za chunusi na chunusi pia zitaanza kupungua kwa kasi kubwa.
Tunakutakia wikiendi njema!