Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

FLP mkuu ni Food Suppliments ambazo zinafanya immune systems ya mwili wako iwe juu, I mean zinafanya kazi kwa kiwango cha juu.

ok! maana hapo juu uliandika "tiba yake ni FLP" ulinistua kidogo nikajua FLP imevuka mstari wa suppliments na kuwa medicine!
 
Unaweza muona daktari wa ngozi,atakupa spot remover au dawa ya pimples....kuna dermatologist mmoja yuko pale dispensary ya UDSM,huduma nzuri,bei chee..jtatu-saturday asbh,ushindwe wewe tu
 
Nikisema Immune system namanisha pia mfumo mzima wa mwili wa binadam unavyofanya kaz. Mfano chunusi na madoa kwenye ngoz hii hutokana na hormone za mwili kutokuwa in balance.
 
Mfano wa hii picha utaweza kuona how FLP zinavyo fanya kaz ktk maswala mazima ya afya ya ngozi na mwili mzima wa binadam.
 

Attachments

  • 1395047550094.jpg
    1395047550094.jpg
    73.7 KB · Views: 225


Je, unapenda kukamua chunusi zilizokuandama usoni ili ziishe? Kama jibu ni ndio, basi acha kufanya hivyo mara moja! Tabia ya kukamua chunusi usoni mara kwa mara yanaweza kukuletea

madhara ya ngozi. Utapata vitundu kwenye ngozi yako ya uso vya kudumu na havitotoka tena kama utaendelea kukamua chunusi (huitwa ‘permanent scarring of your face’). Hata uende kwa

wataalam wa ngozi wanaweza kushindwa kuondoa hizo alama zilizosababishwa na kukamua chunusi. Kukamua chunusi pia kunasababisha ngozi yako kuondokewa na kinga ya kuzuia bacteria ambayo itakusababishia maambukizi mapya na ngozi (severe infections).


Kama inakubidi chunusi zako kuzikamua, basi nenda kwa mtaalam (facial expert) wakaziondoe kwa kutumia vichuma maalum (pimple extractor), anti-bacteria solutions (gel za kuzuia backteria) na lotion au cream ya kutibu chunusi (Acne treatment ointment or cream).


Kama muda au uwezo wa kwenda salon huna, basi tumia maujanja yafuatayo;


1. Acha kukamua chunusi zako hovyo, ukiwa kazini, kwenye daladala, ukiwa ukitazama TV, ukiwa kitandani, na kadhalika. Achana na tabia hiyo maana utajiharibu sura yako!


2. Acha tabia ya kujigusa gusa uso wako kila wakati, hasa kama unazo chunusi tayari


3. Watu wengi wanaopata chunusi wana ngozi za mafuta (Oily skin) hivyo watu hawa wanapaswa kuachana kabisa na vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi. Mfano chipsi, vyakula vya kukaangwa na mapipi, biskuti, nakadhalika. Uamuzi ni wako, chagua kunyoa au kusuka. Utamu wa kuridhisha tumbo/kinywa chako au uso soft.


4. Tumia mafuta au lotion usoni iliyoandikwa 'Oil Free' au 'For Oily Skin'. Ukitumia mafuta yaliyoandikwa 'For Dry Skin' unakuwa unjaiongezea mafuta zaidi kwenye uso wako, hivyo kusababisha uzalishaji wa sebum, ambayo ni chembechembe inayozalisha chunusi.


5. Tengeneza mask mara moja kwa wiki ujifanyie tiba mwenyewe ya asili ukiwa nyumbani. Nunua fungu la majani mabichi ya giligilani (huuzwa sokoni), chambua nusu yake, kisha pima vijiko viwili

vya kulia chakula vya unga wa Manjano. Pondaponda majani ya giligilani (fresh coriander leaves) uchanganye na unga wa manjano (turmeric powder), kamulia na kipande cha ndimu, kisha upake

kwenye chunusi zako na ukae nayo usoni kwa muda wa dakika 10. Kisha nawa uso wako kwa maji ya vuguvugu na upake 'Oil free cream' au lotion yako ya kutibu chunusi. Acne cream and Acne

lotion. Fanya hivi kila wiki kwa muda wa mwezi mzima na utaona alama nyeusi za chunusi na chunusi pia zitaanza kupungua kwa kasi kubwa.

Tunakutakia wikiendi njema!
 

Attachments

  • Blackheads.jpg
    Blackheads.jpg
    11.5 KB · Views: 323
  • blackhead off sheet-1_3.jpg
    blackhead off sheet-1_3.jpg
    18.7 KB · Views: 358
  • black heads.jpg
    black heads.jpg
    16.8 KB · Views: 336
  • onthemove.jpg
    onthemove.jpg
    8.1 KB · Views: 1,126
mkuu. Mzizi mkavu salute sana mkuu.
mimi nina duka la cosmetics nitafuata maelezo yako kuwapa ushauri walengwa
 
Last edited by a moderator:
Asante sana mkuu MziziMkuu kwa darasa zuri. Nina kijana wangu anasumbuliwa sana na chunusi na utafikiri ulimkusudia yeye kwenye maelezo yako ulotoa.Moja kwa moja ninaingia kwenye application ya kutengeneza mask ili aanze kuitumia maana uso wake umeshambuliwa sana na chunuzi. Bigup mkuu.
 
mimi naitaji sana kupona lakin nikitumia bidhaa za limao au ndimu hata zenywe nazidi kuumuka sana na ngozi inazidi kuwa kavuu pia nataman kujua hayo majan ya giligilani yakoje,
 
Ila umesahau kitu kimoja mzizimkavu, wakati mwingine chunusi husababishwa na kukosa kupata choo kikubwa vizuri.
 
Nunua sabuni inaitwa carambola no herbal soap...itakusaidia Sana...siku tatu tu..na hutoa madoa pia..
 
Wadau mimi n kijana wa miaka 21 nahitaji nipate dawa ya kupunguza chunusi na ikiwezekana zipotee kabisa usoni
 
Back
Top Bottom