Hivo vitu vyeupe ni deads skins ambazo zikikutana na hewa sinafanya kama upele fulani hivi au tunaita whiteheads…Unaweza kuviondoa kwa kutumia facial cleansers na oil free moisturizer(cream).
- Osha uso mara mbili kwa siku na maji ya vuguvugu.Baada ya kuosha fanya kama unapigapiga taulo usoni/pat,usisugue.Hii ni njia inayopunguza uchafu na mafuta kujijenga kwenye skin pores.
- Tumia skin cleanser ambayo itaondoa uchafu/deadskin kwenye ngozi.Products kama alpha-hydorxyl acid,salicylic acid au benzoyl-peroxide ni nzuri kwa kuondoa hivo vitu.Ulizia famasi utavipata
- Steaming ni njia nzuri ya kuondoa white heads.Chemsha magi moto weka kwenye bakuli,acha ule mvuke ukupige usoni kwa dakika 15.Steaming ni njia nzuri ya kufungua pores/uwazi za kwenye ngozi,ambapo inakuwa kwa urahisi kuonoda uchafu kwenye ngozi
- Tumia scurbs za aina tofauti kusafisha ngozi ambazo nimezitaja chini
- Ukiosha na kuscrub uso unapoteza moist yote kwa hio ni vyema ukipaka cream ya uso kutokana na aina ya ngozi yako
- Ukitoka kuoga tumia vidole vyako viwili kusugua taratibu eneo la pua ,itaondoa ngozi zote zilizokauka.
- Epuka kujishika eneo hilo wakati wote,kwasababu vijidudu vilivyopo kwenye mikono vinasababisha muongezeko wa hali hio.
Kuna njia mbadala pia ambazo zinaweza kutumia nyumbani kuondoa hizo whiteheads.
- Limau:linasaidia sana kuondoa mafuta na deadskin kwenye ngozi.citric acid iliyopo kwenye limau inasaidia kufungua pores za uso na kuondoa uchafu wote uliokuwepo kwenye pua.Chukua juisi ya limau na sugua kwenye eneo la pua kwa dakika kumi.Rudia hivyo kila siku kwa wiki moja.
- Aloevera:ni anti-septic(inaua vijidudu) in nature na ina anti-oxidants.Changanya drop 3 za juisi ya limau na aloevera gel.weka kwenye uso,kisha sugua taratibu kwa dakika 15,suuza uso na maji moto.
- Nyanya:Nyanya inasemekana kuwa leukopene ambayo ina uchachu unaosaidia kuondoa whiteheads.Tengeneza juisi ya nyanya.Chukua hii juisi na uweke usoni mpaka ikauke.Suuza uso kwa maji ya vuguvugu.
- Asali:Kama una ngozi sensitiv epuka kutumia malimau au nyanya ili uepuka kupata irritation au upele.pasha moto asali yaani kwenye waterbath,ikiwa na joto la kiasi sio la kuunguza,weka usoni na usuge kwenye eneo la pua kwa dakika 10,kisha acha ikauke.Suuza inapokauka.
- Sugar scrub:Saga sukari iwe powder.Changanya na juisi ya limau,weka kwenye eneo la pua na scrub/sugua taratibu .
- Mayai:Mayai yana omega-3 fatacids nyingi,vitamins na minerals ambazo zinamea ngozi.Chukua ule WEUPE wa yai weka kwenye uso,ukishakauka suuza na maji ya vuguvugu.