Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani

Nazidi kuamini maneno ya jamaa mmoja kuhusu hawa watoto waliozaliwa miaka ya 2000. Hawa watoto ni changamoto mno! Hawana adabu wala akili, wao kila wanachofanyia gizani wanataka tusiokuwepo pia tuyafahamu.
Yani waliona ni sifa kabisa kufanyiana mitihani na wangesifiwa kabisa!
 
Issue hapo ni ushahid mzee kumbka hapo ni radio station unaweza kujitapa unakaa masaki na unamiliki range wakati ulikwenda hapo na boda boda toka gongo la mboto
Si wamekiri wenyewe kwa vinywa vyao hahahaha sasa ushahidi gani tena?
 
Wanaweza kusema hiyo kauli waliyotoa ilikuwa ni kuchangamasha tu mahojiano kwenye media waliyokuwepo. Ni ngumu kwa chuo kuthibitisha kuwa mmoja alimfanyia mitihani pacha wake.
 
Hakuna hatua yoyote inayoweza kuchukuliwa.

Ingekuwa sheria za nchi zipo hivyo basi jeshi la polisi lingekamata wanaotoa ushuhuda makanisani.
Sure. Hata watuumiwa wanapokuwa wamekamatwa na kutakiwa kuandika maelezo yao hatimaye uyakana mahakamani na kudai waliyaandika kutokana na undue influence/coercion/intimidation kutoka kwa waliokuwa wakiwachukua maelezo.
 
Hivi kwa kizazi cha sasa mtu aliemaliza Chuo mwaka 2021 kwa sasa atakua na umri gani?! Najaribu kufikiria labda bado ni watoto coz kwa mtu mzima kabsa huwezi kuongea issue kama hii kwenye media hata kama hizo degree hawana kazi nazo. Wanachafua sector ya Elimu na hata wao wenyewe, kwa uropokaji huo ni ngumu kuaminiwa kwenye sensitive issues
 
Degree ni mali ya Chuo na wana mamlaka ya kukunyang'anya muda wowote pale ambapo watagundua kuna walakini.
 
Kuna mwaka kijana mmoja kutoka Ujerumani alifichua kuwa waziri mmoja aliiba tasnifu yake ya master's degree. Yule kijana alimkomalia waziri mpaka waziri akajiuzulu.

Nataka kusema kwamba. Kwa nchi zilizoendelea, mtu akifanya udanganyifu kwenye elimu anajitahidi kuuficha asibainike kwa sababu anajua madhara yake, lakini kwa Tanzania kwa sasa mtu anaona fahari kutrend kwa kuibua kioja bila kujali madhara yake huko mbeleni. Kwa sasa teknolojia inahifadhi, hao wanafunzi watakuja kuumbuka huko mbeleni!
 
Kumbe ndio maana miji yetu haipangiki kwa kuwa wapanga miji na watu wa mazingira wanafanyia mitihani!Tuna shida kubwa!
 
Ni aibu sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…