Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani

Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani

Screenshot_20240307-155319~2.png
 
Tumekuwa tukisikia hapa Duniani hasa Tanzania kuwa huwa kuna degree za bure na wengine wamekuwa wakisema kuna degree za chupi!

Lakini sijawai kusikia au kuona watuhumiwa wakikiri kufanya uhalifu kabisa hadharani!

Chuo cha Ardhi ni chuo kizuri lakini ikifika hatua ya watu kisa tuu mapacha wanaweza kufanyiana mitihani na wana kiri hadharani kuwa walifanyiana mitihani tena ya supplimentary basi ujue hii ni hatua kubwa na dharau kubwa sana kwa taasisi hasa ya Elimu ya juu na inayo aminika!

Hawa mabinti wanasema waliweza kufanyiana mitihani na walimaliza chuo kikuu Ardhi(ARU) mwaka 2021 hakuna aliyegundua na sasa wanakwenda hadharani kusema kuwa waliweza kufanya hivyo ni wazi dharau sana kwa taasisi hii ya Elimu na inathibitisha kuwa taasisi hii haiko makini na kuna walakini kwenye hutoaji wa Elimu!

Watu wana hangaika sana kupata elimu halafu watu wanaidhalilisha elimu kiasi hiki …hii ni aibu kwa chuo cha Ardhi na Wizara ya Elimu pia!

Watu wengi wamekuwa wakitilia mashaka sana Elimu zetu hasa utoaji wake na sasa ni wazi wahalifu wameanza kutoa ushahidi wa mashaka kwenye hizi degree zilizojaa mtaani!

Ni matuamaini yangu taasisi itachukua hatua kali dhidi ya uhalifu huu wa kielemu uliofanywa na hawa mapacha na kwenda kukiri hadharani kwenye chombo cha habari Wasafi FM!

Source: Wasafi FM

View attachment 2926553


Who cares? Watu wote hii nchi wezi tu
 
Aisee imekula kwao,na chuo cha ardhi huwa wapo serious kweli

Nakumbuka nikiwa mwaka wa pili,kuna mwanafunzi alienda kushiriki mashindano ya kutafuta mchumba,then akajitambulisha anatoka chuo cha ardhi,na anasoma architecture, aisee aliwashiwa moto wa kufa mtuView attachment 2927186
Kwa hiyo wanavuliwa degree zao kimchezo mchezo?!
 
WANAWAKE HAWANA SIRI......
NARUDIA TENA WANAWAKE HAWANA SIRI........EXCEPT SIRI MOJA TU NDIO WAGA WANAITUNZA.......NAYO NI IDADI YA WATU WALIO............................ NAO!!!
 
Ila hao mabinti wamewaponza mapacha wengine wanaosoma vyuo vikuu. Watafuatiliwa kwa nguvu Sana. Pia wamewavua nguo Ardhi University kwa huo ujinga
 
Back
Top Bottom