Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Miaka ile ya awamu ya kwanza kulikuwa na chuo cha kufundisha viongozi masuala yote muhimu ya kiuongozi. Kilikuwepo pale kivukoni. Kiliwapika viongozi na matendo yao yakaonekana baada ya kupewa ukuu wa wilaya na ukuu wa mikoa. Walikuwa ni viongozi wenye maadili yasiyohojika.
Taratibu muda ulivyosogea ndio maana ya kile chuo ikiwa inapotea. Wakaanza kupewa vyeo watu wenye kufanya kila aina ya vituko.
Ingawa kwa kusema ukweli siasa za mitandao zikawa chanzo cha kupotea kwa maadili ya kiuongozi. Kupeana nafasi kwa kulipa fadhila ukawa ni mtindo wa maisha ya kisiasa.
Hayati Nyerere aliweza kuwaandaa viongozi ambao waliweza kufanana nae japo kwa kiasi fulani. Waliona ufahari kuwatumikia watu na wakaona ufahari kuwa sehemu ya watu.
Nilimshangaa Mzee wa awamu ya nne pale alipoongelea kujimwambafai kwa wakuu wa mikoa na wilaya wakati wa awamu ya tano, wakati hao aliowasema ni matunda ya ukosefu wa maandalizi ya viongozi kama hali ilivyokuwa wakati chuo cha kivukoni kikiwa katika kilele cha ubora wa ufundishaji wa maadili.
Siasa za mitandao zimeharibu maana pana ya kiongozi kuwa ni mtumishi, zimekuwa ni Siasa za kundi fulani kukaa juu kwenye jamii, na wasio wa kundi hilo wanapambana ili na wao waingie katika kundi la wachaguliwa wachache.
CCM ya JKN ilipigania umoja wa kweli, na viongozi wakafanana na matarajio ya taifa la kistaarabu. Huku kupenda vyeo mpaka watu kuwekeana sumu ndiko kumezalisha hizi siasa za vituko za hawa wanaopewa mamlaka ya kuongoza mikoa na wilaya.
Yule aliyekuwa Dar akijisifu kwamba hakuna anayekula starehe kama yeye asingeweza kuuongoza mkoa miaka ile ya JKN. Yule DC wa Arusha asingeweza hata kufikiriwa kupewa cheo kwa jinsi tabia zake zilivyokosa utu. Huyu aliyepigwa chini Mwanza ni mwendelezo tu wa hawa wanasiasa wa IPhone na Facebook.
Hivyo Mheshimiwa Rais kama ikikupendeza, fikiria namna ya kufufua shule maalum ya kuandaa viongozi, wa sasa wengi wao wanaonyesha kabisa ni matokeo ya makosa ya kutotiliwa maanani maandalizi mazima ya upatikanaji wa viongozi bora.
Mkuu wa mkoa au wilaya sio malaika lakini anaweza kabisa kuwa kioo chema cha jamii anayoiongoza. Hao kina Songambele bado wanazungumzwa na watu wenye umri mkubwa. Kina Jenerali Ulimwengu walikuwa ni viongozi wenye kitu (substance) wanaposimama mbele ya watu.
Mheshimiwa Rais fanya kitu kwenye suala hili, utajiwekea heshima itakayoishi kwenye hisia za wapenda nchi.