A
Anonymous
Guest
Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kina utaratibu mbovu wa kuingia kwenye mfumo unaosimamia taarifa za wanafunzi uitwao SUASIS ambao taarifa za mwanafunzi zinapatikana ikiwemo matokeo, usajili wa kozi, ulipaji ada nk.
Utaratibu uliopo ni kwamba Mwanafunzi hawezi ingia kwenye mfumo huo akiwa nje ya chuo. Ni lazima awepo chuoni. Mfano kwasasa wanafunzi wapo likizo matokeo yakitoka ni lazima mtu harudi chuoni kuangalia matokeo na chuoni lazima utumie internet ya chuo.
Chuo kikubwa lakini Idara ya TEHAMA ni mbovu watu wanateseka sana hata kwenye usajili wa kozi au kupata Control Number za kulipa ada.
Ni tangu semester ya kwanza lakini pia baadhi ya watu waliohitimu miaka ya nyuma wanasema mfumo huo umekuwa ukisumbua kwa muda mrefu. Ukiwauliza wanasema walifanya hivyo ili kuwadhibiti Walimu ambao ukiruhusu uingie kwenye mfumo ukiwa popote basi watajaza taarifa za wanafunzi wakiwa popote pale na wakitakiwa wawepo chuo kwa ajili ya uwasilishaji wa matokeo hawatafika kwakua wana access popote walipo
Semester ya kwanza ilianza Novemba 2025 hadi February 2026 na Semester ya pili March 2026 hadi July 2026. Kifupi matokeo ya semester ya kwanza ilikuwa kuyapata hadi utumie internet ya chuo na sasa hivi hata kuangalia coursework za semester ya pili na kuingia kwenye mfumo huo wa SUASIS hadi uwepo chuoni. Ni vyema wanafunzi wakawa na uwezo wa kuingia wakiwa popote pale.