Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) Acheni Arrogance; Part-Time Teaching Mnafanya Interview? Huko ni kudharau na kudhalilisha Watanzania

Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) Acheni Arrogance; Part-Time Teaching Mnafanya Interview? Huko ni kudharau na kudhalilisha Watanzania

Huu uzi umeandikwa na mtu mpuuzi sana. Vijana acheni uvivu. Yaani hamtaki kabisa kufuata utaratibu matokeo yake mnalialia hovyo
 
Sasa kama waombaji ni wengi, huoni kama ni fair kufanya usaili.

kigezo cha uzoefu ni jambo zuri lakini kwa kufanya hivyo hata wewe uliefundisha miaka 15 utakosa nafasi kama kuna mwingine alifundisha miaka 16 nyuma.

Binafsi sijaona tatizo.

Pengine pendekeza utaratibu maalum

kama ni muda wa kufundisha waandike kabisa tunataka mzoefu wa miaka isiyopungua 15, ili wengine wasiombe.
ila sasa kama ni watu 10 wameomba na wote wamefikisha vigezo na wote wana vyeti vizuri watafanyaje au waandike majina kwenye vikaratasi wafumbe macho wachague kimoja kama bahati nasibu? 😂😂😂
Mkuu, just imagine una miaka 41 alafu unafanyiwa interview na kijana wa miaka 29.
 
mtu tayari umeshafundisha miaka pengine km 15 na zaidi ktk vyuo vingine uje ufanyiwe interview na vitoto vidogo
Mkuu, hii ndio sababu ambayo hata mimi ilinifanya nikaacha kutama job application. Yaaani mimi na ukubwa wangu miaka 37 niende interview chumba kimoja na watoto wa miaka 23? Alafu huyo interviewer mwenyewe ni HR officer binti wa miaka 25 au 27. Seriously? Bora niendelee tu kuuza mahindi ya kuchoma hapa Kitunda.
 
Mkuu, just imagine una miaka 41 alafu unafanyiwa interview na kijana wa miaka 29.
Kama umri ni mali kuliko Kazi, Baki na umri wako.. we Huko ofisin Bosi wako amewapita umri wafanyakazi wote..inshu ni content na uwezo wako unakupa nafasi, Kama wameweka huo utaratibu sidhan kàma nimbaya çoz unakuta mko wengi?? Wanawachagua vipi?? Na hta wakiwachagua bila interview si utakuja hapa jukwaan kulalamika??
 
Mkuu, hii ndio sababu ambayo hata mimi ilinifanya nikaacha kutama job application. Yaaani mimi na ukubwa wangu miaka 37 niende interview chumba kimoja na watoto wa miaka 23? Alafu huyo interviewer mwenyewe ni HR officer binti wa miaka 25 au 27. Seriously? Bora niendelee tu kuuza mahindi ya kuchoma hapa Kitunda.
Kazi njema mkuu.. unahofu ya kushindwa tu? Ungeambiwa we njoo Lazma nikupitishe hao wa Miaka 23 wala usingewawazia
 
Kazi njema mkuu.. unahofu ya kushindwa tu? Ungeambiwa we njoo Lazma nikupitishe hao wa Miaka 23 wala usingewawazia
Hiyo ndio mantiki yangu kwa maana hawa wa miaka 23 bado wanakumbuka walivyokariri darasani, mimi nimesahau vya kukariri, nipo practically. Sasa kwanini nisiogope kushindwa. Eti unaniuliza, what's assets and liabilities, hizi si ni dharau sasa
 
Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) ni chuo kinachomilikiwa na Serikali yetu kupitia wizara ya fedha. Kama ilivyo vyuo vingine vya elimu ya juu na vyuo vikuu wanakuwa na upungufu wa teaching staff(walimu). Tatizo la hawa jamaa ni arrogance yaani kujisikia, majivuni, kujiona wa kipekee wakati ukweli ni kwamba ni chuo cha kawaida kabisa hata siyo Univeristy.

Siku za hivi karibuni walitangaza nafasi kadhaa za part-time, walitaka utume CV na nakala(copies) za vyeti. Sasa cha ajabu eti part-time teaching unataka umfanyie interview mtu ambaye CV yake inaonesha tayari anafundisha aidha ktk chuo kingine cha elimu ya juu au chuo kikuu kingine? Are you serious guys? Kwa kazi ya miezi 4 tu? Mtu atoke Dar Es Salaam, Dodoma,Mwanza au Mbeya kuhudhuria interview siku 2 kwa kazi ya miezi 4?

Kwa hiyo nyie hamuamini vyuo vingine vya elimu ya juu vilivyowaajiri hao wahadhiri? Acheni kiburi na dharau kwa kudhani kuwa watanzania ni maskini kiasi hicho. Msiwanyanyase watanzania kwa kutumia kodi zao wenyewe, hizo pesa ni kodi za watanzania isiwaleweshe.

Nitamshangaa sana mtanzania atakayekubali udhalilishaji huu kwa kuhudhuria hayo ma-interview yao. Watakulipa nini kuzidi utu wako, viwango vyao vinajulikana kwa saa unalipwa sh. 18,000/ jumlisha 10,000/ ya nauli jumla sh. 28,000/. Kwa wiki utafundisha masaa 4 utavuna sh. 112,000/. Semester haizidi wiki 16 ukimaliza vizuri utaambulia sh.1,792,000/. Ukitoa gharama utakazokuwa umetumia plus hii ya interview huna cha maana utakachobakiwa nacho.

Point yangu hasa siyo malipo ni dharau na udhalilishaji eti mtu tayari umeshafundisha miaka pengine km 15 na zaidi ktk vyuo vingine uje ufanyiwe interview na vitoto vidogo kwa kazi ya muda mfupi. Ni vyuo vingi tu vinachukua part-timers hawafanyi upuuzi huu, unawapatia CV yako na pengine unaonesha vyeti au unawaachia nakala za vyeti inatosha. IAA badilikeni enendeni km wenzenu.
Majina wametoa wapi?
 
Kufundisha chuo kingine haimanishi una qualify kufundisha chuoni kwao pia? Nimewahi kufundishwa na doctor (PhD) mmoja kutoka UDOM kama part time alikua haeleweki anafundisha nini mwisho tukalalamika akaondolewa baada ya semista kuisha, Kafanye interview bro
 
Mkuu, hii ndio sababu ambayo hata mimi ilinifanya nikaacha kutama job application. Yaaani mimi na ukubwa wangu miaka 37 niende interview chumba kimoja na watoto wa miaka 23? Alafu huyo interviewer mwenyewe ni HR officer binti wa miaka 25 au 27. Seriously? Bora niendelee tu kuuza mahindi ya kuchoma hapa Kitunda.

Sasa hapa ndipo unapozingua

Unaingiza mambo ya age kwnye mambo ya professsion

Unaeza kuta uyo uli mzidi umri kakuzidi elimu na uwezo vizuri kabisa.

Wao wameweka utaratibu wewe kama unaona huwezi basi achana nao fanya mishe zako.

Mimi ni coordinator wa international organization moja, hata miaka 30 sijafika. Ila interview za part time tunafanyia mpaka wazee wa miaka 50 na nawafanyia mimi na wengineo. Wapo wanaopata na wako wanakosa, kuna vijana wadogo tu wana uwezo mkubwa kuliko wazee. Wacha wapewe kazi
 
Back
Top Bottom