Chuo cha Veta - Njiro Arusha kinatuzungusha tuliosoma Kozi ya Udereva, hawapeleki matokeo yetu kwa TRAFFIC.

Chuo cha Veta - Njiro Arusha kinatuzungusha tuliosoma Kozi ya Udereva, hawapeleki matokeo yetu kwa TRAFFIC.

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
879
Reaction score
814
Chuo cha Veta Kilichopo Njiro Arusha, KOZI YA UDEREVA Ngazi ya (PSV NA VIP) Kimekuwa Kikituzungusha Kutopeleka Matokeo Yetu TRAFFIC.

Wanafunzi wa Intec No. 177 Na 178 Ambao tumesoma mnamo tarehe 24 January 2022, lakini hadi leo ni miaka 4 tukifika Police kwa ajili ya Ku Hakiki Lessen hatuonekani taarifa zetu.

Hata hivyo, tumefuatilia chuoni hapo pasipo mafanikio wakituahidi kuyatuma Matokeo hayo police Bila Kufanya hivyo.

Cha ajabu zaidi!! PSV ambayo tumeunganishiwa Masomo Na VIP unaambiwa Kwenye System tunaona umesoma PSV tu VIP huonekani Na Ada tumelipa Kwa Usahihi.

Tunaomba Mamlaka za juu za Veta kutusaidia Tupate Haki kwani Tulikamilisha Taratibu zote ikiwemo Kulipa Ada, Kujaza Form Na kumaliza Masomo pamoja na Traffic Verification
 

Attachments

  • IMG-20250607-WA0008.jpg
    IMG-20250607-WA0008.jpg
    79.3 KB · Views: 54
Back
Top Bottom