KERO Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kitatoa lini fedha za ‘refund’ tumesubiri tangu Mwaka 2024

KERO Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kitatoa lini fedha za ‘refund’ tumesubiri tangu Mwaka 2024

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ninayo heshima kuwasilisha kero yangu kuhusiana na ucheleweshaji wa kurejeshewa fedha za ada nilizolipa kabla ya kupata mkopo wa elimu ya juu.

Mimi ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology - MUST) wa Mwaka 2024. Kutokana na kuchelewa kupatikana kwa mkopo, nililipa ada yote kwa juhudi binafsi kupitia mzazi/mlezi ili nisiathirike na masomo au kukataliwa kuendelea na masomo.

Baada ya mkopo kupatikana, chuo kilifanya makato ya ada, na hadi sasa kiasi cha Shilingi 210,000/= kimebaki kama salio la fedha nilizolipa awali, ambacho tulielezwa kuwa kingerejeshwa. Hata hivyo, licha ya kufuatilia mara kadhaa, sisi tunaodai tumekuwa tukipewa majibu ya “kusubiri” bila maelezo ya wazi au ratiba maalum ya marejesho.

Baada ya mkopo kupatikana, chuo kilifanya makato ya ada, na hadi sasa kiasi cha shilingi 210,000/= kimebaki kama salio la fedha nilizolipa awali, ambacho tulielezwa kuwa kingerejeshwa. Hata hivyo, licha ya kufuatilia mara kadhaa, tumekuwa tukipewa majibu ya “kusubiri” bila maelezo ya wazi au ratiba maalum ya marejesho.

Sasa imepita takribani miaka miwili, na hadi leo hatujui hatma ya fedha hizo, kama zitarudishwa au la. Hali hii imekuwa kero kubwa kwangu na kwa mzazi/mlezi aliyejitolea kulipa ada hiyo kwa hali ngumu ya kifedha.

Kwa heshima, naomba majibu rasmi na ya wazi kuhusu:

Hatma ya fedha hizo za ada

Lini marejesho yatafanyika

Sababu ya ucheleweshaji wa muda mrefu bila taarifa rasmi

Naomba kero hii ipewe uzito unaostahili ili haki yetu itendeke.
 
Mzee pesa ya serekale usiwe na haraka nayo, utakufa na kihoro. 😁
 
Hili ni tatizo vyuo vyote hata UDOM tumewakaushia lakini lipeni overpayment zetu hela haikosi matumizi
 
Malipo ya refund chuo cha MUST mbeya hayatolewi licha ya kufuata taratibu zote za kiuongozi huku tukiambiwa kwamba anasubiriwa mkuu wa chuo asaini toka mwaka jana hadi sasa hamna kinachoendelea na hakuna taarifa yoyote kwa wanafunzi tunaodai
 
Back
Top Bottom