Chupa zilizojaa mkojo zaidi ya 2,000 zakutwa ndani kwa mama ntilie jijini Arusha

Chupa zilizojaa mkojo zaidi ya 2,000 zakutwa ndani kwa mama ntilie jijini Arusha

Hukohuko kuna yule mwamba alikua na chupa kibao na ndoo kibao kajaza kinyesi.
Na anahojiwa anajibu normal kabisa as if ni kitu ya kawaida.
Sijui huwa wanalala vipi na hiyo.

Dr. Mariposa kikwapa tu kinatukutoa roho, utaweza harufu ya kojo la miaka?? Au ndo ungekuwepo ungewatia mibisu ya tumbo tu.
Mmh! Mkojo wa mtoto tu siwezi kuuvumilia na ndio hata haunuki itakua wa jitu zima,
Watu wana matatizo ya akili, trust me
 
Huko Babati nako siyo shwari
Mwanamke anayefahamika kwa jina la Mama Gifti amekamatwa katika Kitongoji cha Mbugani, eneo la Magugu, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, akidaiwa kufanya vitendo vya ushirikina kwa jirani yake usiku wa kuamkia Agosti 13, 2026.
Mama Gifti anadaiwa kukutwa akiwa bila nguo, akiwa na nyoka pamoja na kisu katika nyumba ya jirani yake, hali iliyosababisha taharuki na wananchi kumkamata kabla ya kukabidhiwa katika vyomba vya ulinzi na usalma.
Tukio hilo limezua hofu miongoni mwa wakazi wa Kitongoji cha Mbugani, huku wananchi wakitaka mwanamke huyo kuhama katika kitongoji hicho kutokana na tabia za ushirikinavilivyobanika.
Viongozi wa serikali ya Kitongoji cha mbugani wamedhibitisha kutokea kwa tukio hilo

View: https://web.facebook.com/reel/845602258520419
 
Kumbe ndo mana chakula chake kilikuwa kitamu vile 🙌
 
Mmh! Mkojo wa mtoto tu siwezi kuuvumilia na ndio hata haunuki itakua wa jitu zima,
Watu wana matatizo ya akili, trust me
Kuna vitu ukifanya mara ya kwanza utajishangaa na kuahidi hutorudia, ila kadri unavyozidi kufanya utaona ni kawaida na utaiaminisha akili yako kua ni sahihi.
 
Back
Top Bottom