kahtaan
JF-Expert Member
- Jul 11, 2009
- 18,760
- 11,343
- Thread starter
-
- #81
Mawazo mazuri na hilo swali anaeweza kujibu ni waziri wa elimu au wa mambo ya nje.mbona picha ya tippu tip sio ya kuchora ni picha ya camera? Picha hiyo sio kama zile za kuchora mwarabu ameshika gobore huku anawaswaga waafrika kwenye msafara wa watumwa. Kwenye vitabu vya historia baadhi ya picha zinaonekana ni za kamera ukiacha zile za kuchora. Tuhitimishe mjadala, sasa kama historia iliandikwa na mkoloni na ipo hukohuko zanzibar pale mji mkongwe, je serikali inaonaje historia hiyo kuendelea kuwepo katika makumbusho yake? La sivyo ijulikane wazi ni kina nani walihusika na biashara ya watumwa
Kwanini historia za UONGO mpk leo zimebaki kwenye maeneo mbali mbali Tanzania?
Na sio hio tu.
Hata wale waitwao watemi wameua sana wananchi.
Kwanini wananchi wasiambiwe ukweli wakajua kuwa watemi walifanya mauwaji kwa wananchi?
Leo watoto wetu wanatunga nyimbo za kuwasifia.
Tunarithishana Ujinga na UONGO.
Ni shida kubwa sana hapa Tanzania.
Wenzetu wa Nchi zingine za africa wamesha amka.
Sisi bado mno.