Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
jk hakuwaahi kuwa mwanafunzi monduli alikuwa mwalimu wa siasa monduli, sijui alipate uafisa, fast tracking ya wasomi jeshini kwa faida ya nani?
Nani kasema JK amewahi kuwa mwanafunzi Monduli?
Waulize wakuu wa majeshi amepata fast tracking kwa faida ya nani. Waulize CCM mfumo mzima wa "chama kushika hatamu" ulikuwa kwa faida ya nani.
Watanzania wamemchagua JK kwa wingi, kwa sababu wengi wetu hatuna utaratibu wa kuhoji, na si tu wengi hatujahoji kupandishana vyeo bila merit, mimi sijawahi kusikia a convinving case for Kikwetes achievements prior to becoming a candidate.
Hivi Kikwete alikuwa na merit gani ya kusema anaweza kuwa rais wa nchi maskini kama Tanzania?
Badala ya kuhoji kwa nini sisi kama jamii hatujahoji JK kukosa merit kabla, na kwa nini tumemchagua licha ya kukosa merit, na kuhoji mfumo mzima wa watu kupanda ngazi bila merit (rais wa pili Ally Hassan Mwinyi alishawahi kujiuzulu Uwaziri wa Mambo ya ndani kwa uzembe kimsingi, akaweza kurudi na kuwa rais hatujaliona hili kama tatizo)
Matatizo yetu hayajaanza na wala hayaishi kwa JK.
Kama tunatafuta suluhisho, tuulize maswali yenye kina cha zaidi ya JK.
Kama vile, ilikuwaje mtu aliyejiuzulu kwa uzembe kama Ally Hassan Mwinyi aweze kupewa nafasi ya kugombea urais? Tena chini ya uangalizi wa kipanga wenu JK Nyerere?
Ukiangalia maswali kama haya utaona huu upuuzi wa kupandishana tu kwa sababu "huyu mwenzetu", hata kama mtu kajiuzulu kwa uzembe, ulianza kabla Kikwete hata hajaingia serikalini.
Kwa hiyo ku focus kwa Kikwete kunaweza kuwa sawa kwa sababu yeye ni rais na yuko visible sana, lakini kuna matatizo yaliyo katika jamii nzima yaliyoanza kabla ya Kikwete na yenye kina kirefu kumshinda Kikwete.
Kikwete si sababu ya matatizo yetu.
Kikwete ni matokeo ya matatizo yetu.
Ukitaka kutatua tatizo kuangalia matokeo ni muhimu, lakini kuangalia sababu ni muhimu zaidi.